Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample
Mtume Paulo anaelekeza kuwa kanisa la Kristo libaki bikira, yaani, liutunze ubikira wake. Mfano wa bikira unalenga uaminifu, utulivu, kujitunza na kubaki na Yesu Kristo daima. Mashaka na kukosa uaminifu huangusha Wakristo na hivyo kanisa. Anguko la mmoja hugusa wengine pia (kumbuka ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa; Mwa 3:1-6, 13). Waalimu wa uongo humfanya mtu akose sifa ya ubikira. Tunawezaje kupambanua mafundisho ya ukweli na uongo? Mistari ifuatayo inaweza kukusaidia kujibu sahihi: Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua(Mt 7:15-22). Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi(Mdo 20:28-31). Kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani(1 Yoh 4:3).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More