Soma Biblia Kila Siku 8Sample
Kwa Israeli si kitendawili kwamba watapata wapi kumjua Mungu kwani neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako (m.14), yaani ameshajifunua kwao kwa njia ya lile Neno walilokwisha kulisikia. Mtume Paulo anakariri mistari hiyo akielezea jinsi ya kuhesabiwa haki kwa imani (Rum 10:6-8: Ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo). Paulo anamaanisha kuwa Kristo hayuko mbali, yu karibu sana, maana yupo katika lile Neno linalohubiriwa. Ndugu, imani, chanzo chake ni kusikia (Rum 10:17: Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo). Imani katika Yesu huja kwa Neno lake.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More