YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 19 OF 31

Uliyebatizwa na kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wako, jua hakika kuwa Yesu Kristo anakuombea kwa Mungu Baba mbinguni!Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea (Rum 8:34). Hutuombea nini? Somo la leo latupa jibu. Anatuombea ulinzi. Tutalindwa kwa kuliitia jina la Yesu Kristo. Mungu atulinde na nini? Atulinde na mafarakano. Yaani Wakristo tuwe na umoja (m.11: Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo). Pili atulinde na yule mwovu, yaani Shetani (m.15: Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu). Halafu anatuombea utakaso. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli (m.17).

Scripture

Day 18Day 20