BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 8 av 20

Katika sehemu hii ya Matendo ya Mitume, ripoti mpya zinawasili zinzoonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la watu wasio Wayahudi wanaomfuata Yesu katika jiji la biashara la Antiokia. Hivyo wanafunzi walio Yerusalemu wanamtuma Barnaba kuangalia kinachofanyika. Anapofika Antiokia, anakuta watu wengi kutoka kote duniani wamejifunza habari za Yesu. Kuna wafuasi wengi wapya na kazi kubwa ya kufanya, hivyo Barnaba anampatia Sauli fursa ya kuja kufundisha naye Antiokia kwa mwaka mmoja.

Antiokia ndiyo sehemu ambapo wafuasi wa Yesu wanaitwa Wakristo kwa mara ya kwanza, kumaanisha “wa Kristo.” Kanisa la Antiokia ndilo jamii ya kimataifa ya Yesu ya kwanza. Sehemu kubwa ya Kanisa haijumuishi Wayahudi wa kimasihi kutoka Yerusalemu tena; sasa ni vuguvugu la makabila mengi linaloenea kwa kasi kote duniani. Rangi za ngozi zao, lugha, na tamaduni ni tofauti, lakini imani yao ni moja, ikiwa na msingi wa habari njema za Mfalme wa mataifa yote, Yesu aliyesulubishwa na kufufuka. Lakini ujumbe wa Kanisa na namna yao mpya ya kuishi inachanganya, na hata kuwa kitisho, kwa mtazamo wa raia wa kawaida wa Rumi. Na Mfalme Herode, mfalme kibaraka wa ufalme wa Kirumi, anaanza kuwatesa na kuwaua Wakristo. Mfalme anavyozidi kuona kuwa kuwatesa Wakristo kunawafurahisha baadhi ya viongozi wa Kiyahudi, ndivyo anavyoendelea kufanya hivyo, jambo ambalo hatimaye linasababisha kukamatwa kwa Petro. Maisha ya Petro yako hatarini, lakini marafiki zake wapo kwenye maombi wakiombea kwa bidii kuachiliwa kwake. Usiku kabla ya siku Herode aliyokuwa amepanga kumtoa Petro kwa umati mkali, malaika anatembelea chumba chake gerezani, anavunja minyororo yake na kumwondoa gerezani.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Ni mawazo, maswali, au maarifa yapi yanajitokeza unaposoma vifungu vilivyoteuliwa vya leo?

• Linganisha Matendo ya Mitume 5:18-25 na Matendo ya Mitume 12:4. Unafikiri ni kwa nini Herode aliamuru vikosi vinne vya wanajeshi kumlinda Petro? Hili linakuambia nini kuhusu Herode na uelewa wake wa hali halisi?

• Jaribu kupata picha upo katika gerezani usiku ambao Ptero aliamshwa na malaika. Unahisi ungelipokeaje hilo? Sasa pata picha kuwa mmoja wa wale waliokuwa wanaombea kuachiliwa kwa Petro. Ungefanya nini Petro alipoanza kubisha mlango?

• Tambua Herode anavyohesimu umati na kutomheshimu Mungu mmoja wa kweli. Linganisha jinsi sura inavyoanza (12:1-4) na jinsi sura inavyoisha (12:22-23) na ufikiri kuhusu kinaya hicho. Pia tafakari na chambua kwa nini na kwa namna gani malaika walijihusisha na simulizi za wahusika katika sura hii (12:7-8 na 12:12:23). Unatambua nini?

• Badili kusoma kwako na tafakari yako kuwa maombi. Mshukuru na utoe heshima na sifa kwa Mungu kwa ajili ya maisha yako. Pia ombea uimara wa Kanisa linaloteswa,tumaini lao, ustahimilivu, na ukombozi.

Dag 7Dag 9

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More