BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve
Katika sehemu hii inayofuata, Luka anaonyesha kuwa kuuliwa kwa huzuni kwa Stefano hakuwezi kusimamisha vuguvugu la Yesu. Kwa kweli, kuteswa huku kunasababisha kutawanyika kwa wanafunzi nje ya Yerusalemu na kwenda maeneo yasiyo ya Kiyahudu yaliyo karibu na Yuda na Samaria. Wanafunzi wanavyoenda nje, wanaleta ujumbe wa Ufalme wa Mungu, kama tu Yesu alivyowaamuru kufanya. Wanafunzi wanatangaza simulizi ya Yesu, na watu wanaachiliwa huru na kuponywa kimiujiza. Mchawi maarufu anaona kuwa uwezo wa Mungu ni mkuu zaidi ya wa kwake, na afisa wa makao ya malkia wa Uhabeshi anabatizwa. Ufalme unaenea na hakuna kinachoweza kuangusha mpango wa Mungu, sio hata mtu anayeitwa Sauli, kiongozi wa dini anayewazoa wafuasi wa Yesu kutoka majumbani kwao na kuwafunga gerezani.
Sauli anaposafiri kwenda Dameski akiwatafuta wanafunzi wengine ili awafunge, anasimamishwa na mwanga unaompofusha na anasikia sauti kutoka mbinguni. Ni Yesu aliyefufuka mwenyewe anamuuliza Sauli ni kwa nini anapigana naye. Kukutana huku na ishara za kushangaza zinazofuata kunabadilisha msimamo wa Sauli kabisa kuhusu Yesu ni nani hasa. Mipango ya Sauli inabadilishwa kabisa. Badala ya kuwatesa wafuasi wa Yesu huko Demeski, Sauli anakuwa mmoja wao na kuanza kumtangaza Yesu kama Mwana wa Mungu mara moja.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
• Pitia mazungumzo ya Petro na mchawi Simoni (tazama 8:18-24). Unatambua nini? Unafikiri ni kwa nini Simoni alimtaka Roho Mtakatifu? Kuna tofauti gani kati ya zawadi na kile kinachonunuliwa? Je, imani ya kuwa unaweza kumchuma au kumnunua Mungu inafananaje na utumwa (8:23)?
• Pitia mazungumzo ya Filipo na afisa wa makao ya kifalme (tazama 8:30-37). Afisa wa makao ya kifalme alikuwa na maswali kuhusu gombo la Isaya, na Filipo alijibu kwa kutangaza habari za Yesu. Lisome gombo mwenyewe na utambue unachoona (tazama Isaya 53). Je, Isaya 53 inamfafanua Yesu vipi?
• Linganisha ufafanuzi wa nia za kusafiri za Sauli (tazama 9:1-2) na kilichomtokea Sauli katika safari yake (tazama 9:20-24). Je, unaona unasaba wowote? Mungu amekubadilisha wewe na mipango yako maishani kivipi?
• Geuza kusoma kwako na tafakari yako kuwa maombi. Ongea na Mungu kuhusu kilichosababisha mshanga wako. Kabidhi mipango yako kwake na umwombe afanye upya ufahamu wako kuhusu utambulisho wake.
Om denne planen
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
More