BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 5 av 20

Ujumbe wa Ufalme unaenea kote Yerusalemu, na idadi ya wanafunzi inaendelea kukua. Wanahitajika viongozi wa ziada, hivyo mwanaume anayeitwa Stefano anajitolea kuwahudumia maskini, mitume wanavyoendelea kutangaza ujumbe wa Yesu. Stefano anaonyesha uwezo na nguvu za Ufalme wa Mungu, na makuhani wengi wa Kiyahudi wanaamini na kuanza kumfuata Yesu. Lakini bado kuna wengi wanaompinga na kubishana na Stefano. Hawawezi kukubali busara ya majibu ya Stefano, kwa hivyo wanatafuta mashahidi wa uongo kumshutumu kuwa amemdharau Musa na kutishia hekalu.

Ili kujibu hilo, Stefano anatoa hotuba thabiti inayosimulia upya simulizi ya Agano la Kale kuonyesha jinsi unyanyasaji wao kwake unafuata mkondo unaotabirika. Anaangazia wahusika kama Yusufu na Musa, watu ambao walikataliwa na kuteswa na watu wao wenyewe. Israeli imekuwa ikikataa wawakilishi wa Mungu kwa karne nyingi, na hivyo si jambo la kushangaza kuwa sasa wanamkataa Stefano. Wanaposikia hili, viongozi wa dini wanashikwa na ghadhabu. Wanamfukuza jijini na kuchukua mawe ili kumpiga hadi afe. Stefano anapoendelea kupigwa mawe, anajitoa kwa dhati kwaYesu, ambaye pia aliteseka kwa sababu ya dhambi za wengine. Stefano anakuwa wa kwanza kati ya wafiadini wengi anapolia akisema, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii."

Soma, Fikiria, kisha Ujibu:

• Soma simulizi mpya ya Agano la Kale ya Stefano. Tambua ni sehemu zipi za Biblia ya Kiebrania alizonukuu na ni maelezo yapi aliyoteua kusisitiza. Unatambua nini?

• Linganisha maneno ya Stefano kuhusu tabia za ukatili dhidi ya manabii (tazama 7:51-52) na ukatili wa wasikilizaji dhidi ya Stefano (tazama 7:57-58). Unatambua nini?

• Linganisha maneno ya huruma ya Yesu kwenye msalaba (tazama Luka 23:34, na 46) na maneno ya huruma ya Stefano wakati wa kifo chake (Matendo ya Mitume 7:60). Unatambua nini? Hili linakuambia nini kuhusu Yesu, wafuasi wake wa kweli, na tabia ya msamaha?

• Je, unamfuata Yesu? Ikiwa unamfuata, kuhubiri ujumbe wake kunaonekana vipi kwako ? Mfano wa ujasiri wa Stefano unakutia moyo au kukupatia changamoto ipi?

• Ruhusu kusoma kwako na tafaakri yako ichochee maombi kutoka moyoni mwako. Muombe Mungu akuonyeshe njia zozote ambazo huenda unamkataa Roho wake Mtakatifu na akusaidie kumfuata badala yeke. Mwambie Yesu hisia zako kuhusu msamaha wake wa huruma kwako na upokee nguvu unazohitaji ili uwasamehe wengine kutoka kwake.

Dag 4Dag 6

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More