BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve
Katika sura za tatu na nne, Luka anatuonyesha jinsi uwezo wa Roho wa Mungu unavyowabadilisha wafuasi wa Yesu kabisa ili kutenda kazi ndani ya Ufalme wake kwa ujasiri. Anaanza na simulizi ya wanafunzi wa Yesu, Petro na Yohana, wanaomponya mwanaume aliyepooza kwa uwezo wa Roho. Wale ambao wanaona muujiza huu wanashangazwa na kuanza kumtazama Petro kana kwamba alifanya hilo kwa uwezo wake mwenyewe. Lakini Petro anaupatia umati changamoto kumtukuza Yesu tu kwa muujiza huu. Pia anahubiri jinsi Yesu alivyokufa na kufufuka tena kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
Petro anajua kwamba watu waliokuwa hekaluni ndio waliomuua Yesu, hivyo anachukua fursa hiyo kuwaalika kubadilisha mawazo yao kuhusu Yesu na kusamehewa. Matokeo yake, maelfu wanaamini ujumbe wa Petro na kuanza kumfuata Yesu. Lakini sio kila mtu. Viongozi wa dini wanakasirika mno wanapoona Petro anahubiri na kuponya katika jina la Yesu, na wanawakamata Petro na Yohana papo hapo. Viongozi wa dini wanadai maelezo kutoka kwa Petro na Yohana ni kwa jinsi gani yule mlemavu alianza kutembea, na Roho Mtakatifu anamwezesha Petro kueleza jinsi jina la Yesu tu ndilo jinalinaloweza kuwaokoa. Viongozi wa dini wanashangazwa wanaposikiliza ujumbe wa Petro na kutahamaki ushupavu wa Yohana. Wanaoa jinsi Petro na Yohana wamebadilika kwa sababu ya Yesu, na hawawezi kukataa muujiza uliofanywa.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
• Petro ni mtu mpya baada ya kushuhudia kufufuka kwa Yesu na kupokea uwezo wa Roho Mtakatifu. Inashangaza! Jionee. Linganisha jibu la Petro kwa wauliza maswali wake kabla ya kupokea Roho Mtakatifu (tazama Luka 22:54-62) na jibu lake baada ya kupokea Roho Mtakatifu (tazama Matendo ya Mitume 4:5-14). Tafakari kwa umakini. Tambua mambo yanayofanana na yaliyo tofauti kati ya maeneo hayo mawili. Unatambua nini?
• Ni kwa njia zipi maalumu Yesu amekubadilisha wewe au mtu yeyote unayemjua?
•Ruhusu kusoma kwako na tafakari ikuchochee kuomba. Ongea na Mungu kuhusu yale yaliyokushangaza, kuwa mkweli kuhusu unachohitaji, na mwalike abadilishe maisha yako.
Om denne planen
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
More