BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Dag 9 av 20

Vifungu vya leo vinaonyesha jambo la kustaajabisha kuhusu huduma ya Yesu. Yesu anasema kuwa yeye ndiye Masihi (Kristo), ila anasema kuwa hatatawala Israeli kama walivyofanya wafalme wengine waliotangulia. Atatawala kwa kuwa mtumishi mwenye kuteseka anayerejelewa kwenye kitabu cha Isaya sura ya 53. Atakufa ili kutwaa enzi yake. Kisha Luka anachambua upekee wa uhalisia huu unaoenda kinyume na matarajio katika simulizi inayofuata.

Katika simjulizi hii, Yesu anawapeleka baadhi ya wanafunzi wake mlimani, ambako uwepo tukufu wa Mungu unaonekana kama wingu linalong'aa naye Yesu ghafla anabadilika. Watu wengine wawili wanajitokeza, Musa na Eliya, manabii wawili wa kale ambao pia utukufu wa Mungu umewashukia mlimani. Mungu ananena kwenye wingu akisema, “Huyu ni mwanangu, msikilizeni.” Hili ni tukio la kustaajabisha! Kisha Luka anatueleza kuwa Yesu, Eliya na Musa wanazungumza kuhusu kuondoka au “kutoka” kwa Yesu. Luka anatumia neno la Kigiriki exodos (neno linalotumiwa na Wagiriki kurejelea kifo) kama njia ya kuonyesha uhusiano kati ya atakalotenda Yesu Yerusalemu, na kutoka kwa Waisraeli nchini Misri. Kwa hili, Luka anatuonyesha kuwa Yesu ndiye nabii mkuu zaidi. Yeye ndiye Musa wa kizazi kipya ambaye, kupitia kuondoka kwake (kifo), atawakomboa Israeli kutoka kwenye ufalme wa dhambi na maovu yote.

Na baada ya ufunuo huo wa kushangaza, huduma ya Yesu huko Galilaya inakamilika, kisha Luka anaanza simulizi kuhusu safari ndefu ya Yesu kuelekea mji mkuu ambako atakufa ili kutawazwa kuwa mfalme wa kweli wa Israeli.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Linganisha unabii kwenye kitabu cha Isaya sura ya 53 na maneno ya Yesu kuhusu atakavyotawazwa kumiliki enzi ya Israeli (9:20-25). Unatambua nini?

•Linganisha maneno ya Mungu kwenye wingu linalong'aa (9:35) na maneno Yake kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati 18:15-19. Unagunduanini?

•Walio wa falme za dunia hii wanaepuka mateso ili kupata kisichowezwa kudumu kwenye nafsi zao. Lakini Yesu alisema kuwa walio wa Ufalme wake wanateseka kwa hiari wanapofuata maneno yake yenye uzima na kwamba hakuna kitu cha faida zaidi kuliko hili! Je, unachukulia vipi Ufalme wa kipekee wa Yesu? Je, umejifunza nini kuhusu kunyenyekea (9:46-50), kukubalika na watu (9:51-56), faraja na mazoea (9:57-60) unapomfuata na kumsikiliza Yesu?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Staajabia mpango wa ajabu wa Mungu, kiri kuhusu masumbuko yako na umwombe akuwezeshe kumfuata licha ya mateso.

Dag 8Dag 10

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More