BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve
Injili ya Luka inaishia na Yesu akiwa na wanafunzi wake wote wanashiriki chakula kingine. Kila mmoja wao anashangazwa na mwili wake uliofufuka. Wanaona kuwa yeye bado ni mwanadamu, lakini pia ni mkuu zaidi. Amekufa na akafufuka akiwa na mwili mpya. Kisha Yesu anawaeleza habari hii ya kustaajabisha. Atawapa uwezo ule ule wa kiungu uliompa nguvu, ili waweze kwenda na kushiriki habari njema ya Ufalme wake na watu wengine. Baada ya haya, Luka anatueleza kuwa Yesu alipaa kwenda Mbinguni, ambako Wayahudi wanaamini kuwa kiti cha enzi cha Mungu kipo. Wafuasi wa Yesu wanaendelea kumwabudu Yesu. Wanarejea Yerusalemu na wanasubiri kwa furaha nguvu ya kiungu ambayo Yesu aliahidi. Kisha Luka anaendelea na simulizi hili katika barua yake inayofuata, kitabu cha Matendo ya Mitume. Ni kwenye kitabu hiki ambapo anaelezea simulizi ya kusisimua kuhusu jinsi wafuasi wa Yesu walivyopokea nguvu za Mungu na kueneza habari njema ulimwenguni.
Jibu:
•Hebu fikiria ungekuwepo siku Yesu alipopaa kwenda mbinguni. Je, ungejisikiaje? Ungesema na kufanya nini?
•Je, unaamini kuwa Yesu ndiye Mfalme wa kweli, na Ufalme wake ni habari njema? Unaweza kushiriki hili na nani? Unaweza kualika mtu mmoja au wawili wajiunge nawe kusoma mwongozo huu. Utaelewa zaidi utakaposoma mara ya pili, na utaweza kushiriki na marafiki yale uliyojifunza. Tungependa kusikia kutoka kwako.
•Je, unaweza kuwapendekezea wengine mwongozo huu wa kusoma? Je, kipi kilikuvutia zaidi katika siku hizi 20 zilizopita? Tueleze kupitia mitandao wa kijamii ukitumia heshitegi #BibleProjectUpsideDownKingdom. (do not translate)
Anza Ufalme Unoenda Kinyume na Mataraijio sehemu ya pili.
•Jiunge na BibleProject katika sehemu ya pili ya Ufalme Unoenda Kinyume na Mataraijio, ambapo tutachambua kitabu cha Matendo ya Mitume. Alika mfanyakazi mwenzako, jirani, rafiki, au mwanafamilia ajiunge nawe.
Skriften
Om denne planen
Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.
More