BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Dag 18 av 20

Viongozi wa hekalu hawawezi kumuua Yesu bila ruhusa ya gavana wa Kirumi, Pontio Pilato. Kwa hivyo wanamshtaki Yesu kuwa yeye ni mfalme mwasi anayechochea mapinduzi dhidi ya mtawala wa Kirumi. Pilato anamwuliza Yesu, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu anamjibu, “Wewe wasema.” Pilato anaona kuwa Yesu hana hatia na hastahili kifo, lakini viongozi wa kidini wanasisitiza kwamba Yesu ni mtu hatari. Kwa hivyo baada ya Yesu kupelekwa kwa Herode kisha kurudishwa kwa Pilato akiwa amejeruhiwa na anatokwa na damu, wanakubaliana jambo la kushangaza. Pilato atamwachilia mwasi halisi wa Rumi, anayeitwa Baraba, badala ya Yesu. Asiye na makosa anahukumiwa badala ya mwenye hatia.

Yesu anachukuliwa pamoja na wahalifu wengine wawili walioshtakiwa na anasulubiwa kwa misumari kwenye msalaba wa Warumi. Kifo chake kinafanywa hadharani. Watu wanapiga mnada nguo zake na kumdhihaki wakisema, “ikiwa wewe ndiye Mfalme wa kimasihi, jiokoe!” Lakini Yesu anawapenda adui zake hadi mwisho. Anawaombea msamaha waliomsulubisha na anampa tumaini mmoja wa wahalifu waliosulubishwa pamoja naye akisema, “Leo utakuwa nami paradiso.”

Ghafla giza linafunika nchi yote, pazia la hekalu linapasuka katikati, na Yesu anamlilia Mungu kwa pumzi yake ya mwisho, “mikononi mwako naiweka roho yangu.” Jemadari wa Kirumi anashuhudia haya yote na kusema, “hakika mtu huyu alikuwa mwenye haki.”

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Je, umejifunza nini leo kutokana na simulizi ya Luka kuhusu kifo cha Yesu?

•Linganisha hukumu ya Pilato na Herode ya kumzuia Yesu asiuawe na juhudi za umati wa watu wa dini wanaotaka auawe. Unaona nini? Unapofikiria kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Yesu (kifungu cha 23:2), mashtaka haya ni kinzani kwa namna gani? •Chambua mazungumzo kati ya wahalifu (soma 23:39-43). Unatambua nini? Je, unajifunza nini unapozingatia jinsi Yesu alivyojibu ombi la mhalifu? Unaposoma kuhusu mazungumzo haya, unajifunza nini kuhusu Ufalme wa Yesu?

•Luka anatueleza kuhusu kiongozi mmoja wa kidini aliyeitwa Yusufu ambaye alipinga mpango wa wenzake wa kumsulubisha Yesu (kifungu cha 23:50-51, 22:66-71, 23:1). Fikiria jinsi Yusufu anavyoonyesha upendo wake kwa Yesu (soma 23:52-53). Je, wewe ni mwanachama ya kikundi usichokubaliana nacho? Na Je, unaweza kuonyesha vipi kile unachoamini?

•Pilato, Herode, umati unaoomboleza na umati unaodhihaki, Simoni, viongozi wa kidini waliopanga njama na Yusufu anayepinga njama, mhalifu upande wa kushoto wa Yesu na mhalifu upande wake wa kulia, wote wamehusishwa na Yesu kwa njia tofauti. Je, ni mhusika au wahusika wepi unaojifunza mengi zaidi kutokana nao?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kumwomba Mungu kutoka moyoni sasa. Anasikiliza.

Skriften

Dag 17Dag 19

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More