BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Dag 8 av 20

Luka anatueleza kwamba Yesu anaanza kutangaza Ufalme wa Mungu mijini na vijini. Lakini badala ya kusafiri kwa msafara wa kifalme kama mfalme wa kawaida, Yesu anasafiri na wanafunzi wake kumi na wawili wasio na hadhi ya juu pamoja na wanawake aliowaponya na kuwaweka huru. Na wanaoandamana na Yesu sio wafuasi tu; ni watendakazi pamoja naye. Wale walioipokea habari njema ya Yesu, ukombozi na uponyaji ndio walioieneza injili kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Safari zao zilijaa milima na mabonde. Yesu anatuliza dhoruba, anamkomboa mtu kutoka kwenye kifungo cha maelfu ya mapepo, anamponya mwanamke aliyepinda mgongo kwa miaka kumi na miwili, anamfufua msichana wa miaka kumi na miwili na anawalisha maelfu ya watu kwa chakula cha mvulana mmoja––baada ya watu wote kula, chakula kilichobaki kinajaza vikapu kumi na viwili!

Unaposoma kifungu cha leo, ona jinsi Luka anavyorudia neno “kumi na mbili” mara kadhaa. Kumbuka, Yesu aliwachagua kimakusudi wanafunzi kumi na wawili kuonyesha kuwa anafanya mageuzi ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Luka anaangazia hili, hivyo anarudia neno “kumi na mbili” mara kumi na mbili kwenye simulizi yake ya Injili. Kila anapotumia neno hili, anaonyesha njia nyingine ambayo Yesu anakomboa makabila kumi na mawili ya Israeli, na kupitia Israeli, ulimwengu wote.

Mungu aliahidi kwamba kupitia makabila kumi na mawili ya Israeli mataifa yote yatabarikiwa, na Mungu aliwaita Israeli kuwa nuru kwa mataifa yote. Israeli hawakutimiza amri waliyopewa, lakini Mungu ni mwaminifu kutimiza ahadi zake. Yesu anakuja kurejesha mwito wa Israeli wa kuwa baraka kwa ulimwengu, na anafanya hivyo kwa kuwatuma wanafunzi wake kumi na wawili kutangaza Ufalme wa Mungu.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Wanaopokea habari njema ya Masihi (Isaya 61:1-3) ndio wanaoieneza ili “kujenga upya miji iliyoharibika” (Isaya 1:4). Chambua tena uhusiano ulipo kati ya Isaya sura ya 61 na maandiko haya ya Luka. Unatambua nini?

•Soma Isaya 42:6-7. Tafakari kuhusu mpango wa Yehova wa kuiteua Israeli kuwa nuru ya mataifa. Unaona nini?

•Yesu anafundisha kwa mafumbo ili kufafanua jinsi Ufalme wa Mungu unavyopokelewa. Kama mbegu, unaweza kupokelewa vizuri na kutoa mazao mengi, au unaweza kuwekewa vikwazo hivyo usiweze kushamiri. Kama mwanga wa taa, unaweza kuonyeshwa ili wote waupokee, au unaweza kufichwa. Walio wa familia ya Yesu ni wale wanaopokea neno la Mungu na kuchukua hatua ili kuubariki ulimwengu (Luka 8:21). Je, umepokea vipi Ufalme wa Mungu? Je, kuna vikwazo, wasiwasi au vishawishi vyovyote vinavyokuvuta mbali na Yesu na kazi yake ya kuubariki ulimwengu?

Kutafakari kwako kukuchochee kumwomba Mungu. Nena na Mungu kuhusu kushawishika kwako, jinsi unavyokubaliana na anayosema, kinachokuzuia kushiriki habari njema, na unachohitaji.

Dag 7Dag 9

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More