BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaPrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Dag 6 av 20

Yesu anawateua wanaume kumi na wawili miongoni mwa wanafunzi wake wote kuwa viongozi, nambari kumi na mbili sio nasibu. Yesu anawachagua wanaume kumi na wawili kimakusudi kuonyesha kuwa anakomboa makabila kumi na mawili ya Israeli kwa kuunda kabila jipya. Ila kwa kutazama kwa haraka, Israeli hii mpya haionekani kuwa bora kuliko ile ya awali. Yesu anawachagua watu kwa mchanganyiko usioleweka kabisa, kuna wasomi na wasio na elimu, matajiri na maskini. Yesu hata anamchagua mtoza ushuru aliyefanyia kazi utawala wa Warumi na pia anamteua mwasi (mtu wenye itikadi kali) aliyepigana dhidi ya utawala wa Warumi! Upendo wa Mungu kwa maskini na wageni huwaleta pamoja watu wasiopatana. Inaonekana kana kwamba kamwe hawatapatana, lakini maadui hawa wakubwa wanaacha shughuli zao zote na kumfuata Yesu na kuingia katika utaratibu mpya wa kuendesha ulimwengu, wanapatanishwa na kuishi kwa umoja.

Luka anatuonyesha kilichoko kwenye utaratibu huu mpya wa kuendesha ulimwengu katika simulizi yake ya mafundisho ya Yesu kuhusu Ufalme unaoenda kinyume na matarajio. Katika mafundisho yake, Yesu anasema kuwa maskini wamebarikiwa kwa sababu wana Ufalme wa Mungu, na kwamba wale wanaolia sasa watafurahi siku moja. Katika utaratibu mpya wa kuendesha ulimwengu, wafuasi wa Yesu wanapaswa kuwapenda adui zao, kuwa wakarimu kwa watu wasiowapenda, kuwa wenye fadhili na kusamehe. Yesu hakuzungumzia tu kuhusu njia hii ya kuishi. Alionyesha mfano na akawapenda adui zake kwa kutoa dhabihu iliyo kuu zaidi–– kutoa maisha yake.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Je, Yesu ulikuchagua pamoja na mtu usiyempenda? Je, mafundisho ya Yesu ya Ufalme unaoenda kinyume na matarijio (Luka 6:20-38) yanasema nini kuhusu uhusiano huo? Je, ni hatua gani unaweza kuchukua kumwonyesha fadhili na upendo mtu usiyempenda?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Pokea fadhili za Yesu unapowaombea wengine kupata fadhili zake. Fungua moyo wako umweleze kwa ukweli na uwazi msaada unaohitaji kuhusiana na hili. Anakusikiliza.

Dag 5Dag 7

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More