Muda wa kupumua Mfano
Pesa si pesa tu kwa Mungu. Ni zaidi ya shilingi na senti na mikopo na bajeti. Kwa Mungu, matumizi yako pesa yako inaonyesha kipendacho roho. Jinsi unavyoitumia (ama kama tunavyoona leo, iwapo uko tayari kutoitumia) inamwonyesha Mungu jinsi uko tayari kujitolea ili kumfuata. Hii ndiyo maana kuwa na mipaka—ama muda wa kupumua—si njia bora zaidi ya kusimamia kalenda yako pekee, bali pia ni njia bora zaidi ya kusimamia pesa zako.
Kusimamia pesa zako na mipaka ina maana gani? Inamaanisha kwamba hutumii pesa zako zote. Unawacha muda wa kupumua kati ya pesa unazopata na pesa unazotumia. Mstari wa leo kutoka Luka unaeleza mbona jinsi unavyotunza pesa yako ni muhimu sana kwa Mungu. Katika mwisho wa mbazi ndefu, Yesu anahakikisha kwamba wasikilizaji wake wanaelewa maana ya mbazi yake kwa kusema, “Huwezi kuwatumikia mabwana wawili . . . Huwezi kutumikia Mungu na pesa.” Karne mbili zilizopita, wasikilizaji wake Yesu wangeweza kugeuka watumwa kwa sababu ya kutolipa deni. Leo, bwana wako anaweza kuwa kadi ama kampuni la mikopo. Hata hivyo matokeo ni yale yale: mtu mwengine anakutawala.
Pengine Mungu anakuhimiza uhamie mji mwingine, lakini ikiwa una mkopo wa nyumba yako na huwezi kuiuza, huna uhuru wa kufanya jinsi Mungu alivyokuagiza. Yamkini anakuita uchukue mtoto wa kupanga, lakini umetumia pesa yako yote badala ya kuiweka na huwezi kumchukua mtoto kwa sababu huna pesa, basi huna uhuru wa kumfuata Mungu. Ama labda unahisi unafaa kuacha kazi yako, lakini familia yako itaathirika ukiwacha kazi yako kwani unatumia pesa yako yote unayolipwa.
Jinsi unavyoweka pesa zako ni muhimu kwa Mungu kwa sababu pesa yako inaweza kukuzuia kusema ndio kwa yale anayokuita ufanye.
Hii ndiyo maana unahitaji muda wa kupumua katika pesa yako. Kutunza pesa zako na mipaka (yaani, kutokuwa na madeni, kutumia pesa yako kwa busara, kuishi maisha ya wastani) inakupa uhuru wa kuwa mkarimu, kuwatumikia wengine, kusema ndio anapozungumza go. Inakupa uhuru wa kufuata Mungu akikuongoza katika maisha bora zaidi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa... Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.
More