Muda wa kupumua Mfano
Siku zetu zimejaa na mikutano, matukio, wajibu, kuchukua watoto, kuchunga wazazi, kuwahudumia watu wengine, kutafuta “wakati wangu,” kufanya shughuli, kuenda mtaani, kuchoka tiki, na kuishiwa na nguvu . . . Wakati mwingine ningependa “kujilaza katika malisho ya majani mabichi ,” ama kuketi “kando ya maji matulivu.” (Ingawa nitatosheka na kikombe cha kahawa katika varanda ya nyuma. Wewe pia?)
Tunahitaji muda wa kupumua.
Muda wa kupumua ni nafasi kati ya mwendo wako na mwisho wa uwezo wako. Muda wa kupumua ni kupiga soga na rafiki yako wa dhati. Muda wa kupumua ni kula chajio mezani wala si katika gari kutoka mkahawa. Muda wa kupumua ni uwezo wa kupeana kwa wingi kwani hujatumia pesa yako yote. Muda wa kupumua ni maisha ambayo ni wa mwendo polepole kimakusudi na ambayo mambo muhimu yamepewa kipaumbele kimakusudi.
Najua kwamba utakubali kwamba kuishi kwa namna hiyo ni bora kuliko wasiwasi unaotokana na kuwa na majukumu mengi usiyoweza kutimiza. Hata hivyo, ukiangalia vitu ambavyo unafaa kufanya ama ukiangalia kalenda yako utaona kwamba—kama sisi wengine—ni ngumu kupunguza mwendo wako.
Kwa hivyo, ni nini inakufanya uishi zaidi ya uwezo wako?
Ni ngumu kutambua na kukiri, lakini kwangu, ni hofu. Ninaogopa kwamba nitakosa, kwa hivyo ninajaribu kupata wakati wa kula chajio na marafiki zangu hata ingawa nimechoka. Ninaogopa kwamba nitaachwa nyuma, kwa hivyo nasakura ili kutafuta gari jipya ingawa hakuna shida na gari ambalo ninalo. Ninaogopa kusikitisha watu, kwa hivyo ninakubali kujiunga na jopo hilo ingawa sijali kuhusu mradi unaotekelzwa . . . unatambua haya?
Hofu inatudanganya kwamba tunakosa na kuachwa nyuma, kwa hivyo tunajaza kalenda zetu na kufilisi pesa zetu. Hofu inaiba muda wetu wa kupumua. Lakini, unajua amri lililorudiwa zaidi katika Biblia? Usiogope. Mungu anatuambia kwamba hakuna haja hofu ituambie mambo ya kufanya. Anatupa njia rahisi ya kuondokana na hofu.
Kesho tutaangalia njia ambayo Mungu amekuwa akitualika (kwa miaka na mikaka) tuwe na muda wa kupumua maishani mwetu. Ukisubiri, angalia kalenda yako na ujiulize: Ni jambo lipi ambalo nimekubali kuhudhuria kwa sababu uliogopa kuachwa nyuma au kusikitisha mtu kwa kukataa?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa... Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.
More