Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Muda wa kupumua Mfano

Breathing Room

SIKU 2 YA 5

Si lazima uwe mwamini ili kujua kuhusu ama kushiriki katika Sabato—siku ya kupumzika. Sote tunapenda siku ya wikendi ambayo huna chochote cha kufanya, labda usiamke mapema, kupumzika baada ya kutia bidii kazini. Lakini ukiona Sabato kuwa Jumapili wa utulivu pekee, unakosa kutambua sehemu bora zaidi—sehemu ambayo itakupa muda wa kupumua.  

Turudi kidogo katika hadithi ambayo inatuleta kwa somo la leo kutoka kitabu cha Kutoka ambapo Mungu anawajulisha watu wake kuhusu Sabato. Waisraeli walikuwa watumwa Misri kwa miaka 400, wakifanya kazi siku nzima, kila siku. Kisha wanaachiliwa huru na taifa zima linazurura jangwani kwa miaka zaidi ya 40. Na ni hapa ambapo Mungu anawapa amri ya kufuata Sabato—kupumzika siku moja katika wiki. 

Mungu anawaambia watu ambao walikuwa wakifanya kazi kila mara kwa miaka na mikaka na ambao wanajaribu kupata chakula cha kutosha kuwalisha watu maelfu walio jangwani kwamba wanafaa kupumzika siku moja. Lazima walifikiri kwamba ni wazimu! Ikiwa hawakufanya kazi siku hiyo, hawangekula siku hiyo.

Hata hivyo, Mungu alikuwa na mpango. Katika Kutoka 31:13, anaeleza kwamba kufuata Sabato itakuwa ishara kwa Waisraeli kwamba “Mimi ni Bwana…” Mungu alikuwa akiwaambia (na kutuambia), Nataka kukuonyesha kwamba ninaweza kuaminika. Najua kwamba unaogopa kwamba utalala njaa. Lakini nitathibitisha, wiki baada ya wiki, kwamba ninaweza kuaminika.

Labda unajua hadithi yote. Mungu alitumia mana na kware kutuliza hofu yao ya njaa kwani aliwapa kila siku na kuhakikisha kwamba walipata cha kutosha hata katika siku aliyowaambia kupumzikak.

Amri la Mungu kwamba tupumzike ni mwaliko tuweke tumaini letu kwake. Tunapoogopa kukataa mwaliko kwani tutamwumiza rafiki yetu, tutaamini kwamba Mungu atalinda urafiki huo. Tunapohofia kwamba nyumba yetu ni ndogo sana, ama gari letu ni kuukuuu zaidi, ama nguo zetu si maridadi, tunaweza kuweka imani yetu kwa Mungu kwamba thamani yetu si katika mali. Kuweka imani yetu kwa Mungu badala ya kukabiliana na hali au kujitahidi hata zaidi ya uwezo wako ndio njia ya kupata muda wa kupumua wa kudumu.  

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Breathing Room

Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa... Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Sandra Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://breathingroom.org