Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Muda wa kupumua Mfano

Breathing Room

SIKU 3 YA 5

Ikiwa umengoja siku ya kuzaliwa, umesomea mtihani wa mwisho, umeolewa, umepata mtoto, ama umesheherekea Krismasi, basi “umehesabu siku zako.” Ulijua kwa uhakika siku ambazo ulibaki nazo kununua vitu, kusoma, ama mpaka sherehe yako ifike ingawa pengine hukuiita kuhesabu siku zako. 

Katika mstari wa leo ambao unatoka Zaburi 90, Musa anamwomba Mungu atusaidie tuishi kila siku kana kwamba kuna tarehe ya mwisho ya kufanya vitu—“kutufunza tuhesabu siku zetu” kwani hii hutupa uwazi wa mambo. Ikiwa kumebaki siku tatu pekee ili Krismasi ifike na bado una zawadi kununua, hutazembea kochini ukitazama runinga. Una mambo muhimu zaidi ya kufanya. Kujua kwambo una muda wako una mipaka unakulazimisha kuweka mipaka kwa mambo ambayo unafanya katika wakati wako.

Kamwe kutakuwa na sherehe za kuhudhuria, miradi ya kutekeleza, majopo ya kujiunga nayo, ziara za kuzuru, na shughuli ndogondogo za kufanya. Na hofu itakuambia kwamba heri ufanya hayo yote ama utafeli. Lakini kuhesabu siku zako ni kama kuweka kichungi kwa mambo haya yote. Ni njia ya kupa kipaumbele mambo na watu walio muhimu zaidi.

Jopo ambalo ulijiunga nalo kwa sababu ya hofu kwamba usipojiunga nalo utakuwa ukitenda hatia? Halitoshi. Ziara ya kazi ambayo itakutenga na watoto wako kwa wiki nzima? Kwa sasa, la.

Tukianza kufahamu kwamba tuna muda mfupi, tutafanya maamuzi ya busara kuhusu vitu, na muhimu zaidi watu, ambao wanastahili kupewa wakati wetu mfupi.  Musa anasema kwamba “tutakuwa wenye hekima.” Ikiwa kalenda yako imejaa, una mambo mengi zaidi ya kufanya, ama umechoka sana, jaribu kuhesabu siku zako. Kiri kwamba (hata ingawa unatumaini kuendelea kuishi kwa miaka mengi zaidi) muda wako ni mfupi, kwa hivyo ni lazima upunguze vitu ambavyo unafanya katika wakati wako. Nakuahidi kwamba unapoweka kichungi hicho, utapata huo muda wa kupumua katika kalenda yako ambao umekuwa ukitamani. 

Kesho tutaangalia kichungi kingine ambacho utakupa muda wa kupumua katika pesa zako. Ukingoja, jiulize: Ni kitu gani ambacho sitaki kuendelea kufanya katika wakati wangu mfupi?  

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Breathing Room

Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa... Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Sandra Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://breathingroom.org