Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii Mfano
Siku ya Tano: Tumainia Uaminifu Wake:
“Unaniamini?”
Swali hili linatukabili kila siku, kutoka wakati tunaamka hadi tunapolala. Kwa sababu kutumaini ina maana ya kupumzika, na kupumzika ni kutumaini.
Hebu fikiria: Hutaweka mti wa Krismasi katika kinara ambacho knakosa mguu mmoja, na hutauliza mtu anayependa kuchelewa alete kichangamsha kinywa cha kula kabla ya chakula maalum.
Haijalishi iwapo tunautambua ama hatutambui, lakini tunatathmini uaminifu wa vitu na watu kila mara. Na tunafanya vivyo hivyo na uhusiano wetu na Mungu, tukijadili kisiri kiasi ambacho tutamwaminia.
Inaweza kuwa mali yetu, uhusiano uliovunjika, machungu yaliyofichika, ama ndoto za siku za usoni, lakini tunatathmini uaminifu wa Mungu kulingana na siku zilizopita ili kuamua iwapo tunaweza kumwamini katika wakati uliopo.
Lakini ni katikati ya shughuli za sherehe ambapo kuamini kwetu ama kutuoamini kwetu kunadhihirika wazi.
…Tutakula biskuti, mahamri na kiga cha likizo mpaka tushibe ikiwa hatutamwamini Yesu kuwaMkate wa Uzima anayetushibisha.
…Tutakuwa na wasiwasi kuhusu mwana mpotevu iwapo hatutamwamwini Yesu kuwa Mchungaji Mwema anayemrejesha nyumbani kondoo aliyepotea.
…Tutajihurumia katika upweke, na kuhisi tumesahauliwa, ikiwa hatutamwamini Yesu awe Imanueli , Mungu anayeishi nasi hata kama tuko peke yetu.
…Tutajitahidi kutengeneza Krismasi iliyokamilika ikiwa hatutamwamini Yesu kuwa Mtakatifu wa Mungu anayetukamilisha.
Kila wakati ni nafasi mpya ya kutumainia uaminifu wa Mungu kwa njia mbalimbali, na inaanza kwa kujua kupumzika.
Ingekuwaje ikiwa badala ya kuanza siku zetu ghafla na shughuli, tungeanza kila asubuhi na mazoezi rahisi ya kupumzika? Tuagize, kama mwandishi wa zaburi, roho zetu kupata pumziko kwake pekee: kukumbuka matendo yake na wema wake, kudhihirisha uhitaji wetu, kutuliza akili zetu na mioyo yetu katika uwepo wake, kutangaza uhakikisho wetu katika uaminifu wake.
Kwa sababu yeye aliyeumba ulimwengu ingawa alikuja kama kitoto kichanga huo usiku mtakatifu, tunaweza kunena utulivu na amani maishani mwetu leo.
Maswali ya Kutafakari: Ni jina lipi la Yesu linalokunenea kuhusu changamoto unazokabiliana nazo maishani mwako? Kumwamini Mungu na kupumzika kwake ina maana gani kwako msimu huu wa Krismasi? Utafanya nini tofauti?
Unataka zaidi? Pakua kifungu cha Kufungua Majina ya Yesu(Unwrapping the Names of Jesus) na utapokea shajara ya maombi ya Majina ya Yesu (Names of Jesus), Alamisho ya Kitabu ya Maombi ya Pumziko(Rest), na Ombi la Pumziko la Krismasi (Prayer for Christmas Rest) unaoweza kuchapishwa.
Kuhusu Mpango huu
‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda. Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo kutoka Biblia kuhusu Ujio (Unwrapping the Names of Jesus: An Advent Devotional) na utakuongoza kupokea pumziko la Yesu Krismasi huu kwa kuchukua muda kukumbuka wema wake, kudhihirisha uhitaji wako, kutafuta utulivu wake, na kutumainia uaminifu wake.
More