Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii Mfano

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

SIKU 1 YA 5

Siku ya Kwanza: Mbona tunahitaji Pumziko wakati wa Krismasi

“Pamba nyumba,” ni maneno ya kwanza ya wimbo huo wa Krimasi unaojulikana na wengi. Na tunafanya hivyo. 

Wengine wetu wanaaanza kujitayarisha kwa Krismasi ikikaribia msimu huo, ilhali wengine wanaahirisha mipango mpaka mwisho. 

Lakini wakati mmoja au mwingine tunakuwa na mambo mengi ya kufanya—mengi yanaleta raha lakini bado yachosha, na roho zetu zinaachwa zimejaa na pia zi tupu. Aghalabu, ni katikati ya sherehe kama hizi ambapo tunafikiria, “Ni haya tu?” Habari njema ni kuwa zaidi ya chakula, ununuzi, na mapambo kuna Mwana wa Mungu aliyekuwa mwanadamu kwa ajili yetu.

Mungu anajua kwamba tuna mwelekeo wa kufanya mambo mengi kwa msisimko. Hii ni sababu moja yake ya kutengeneza siku la kupumzika kwa Wanaisraeli baada ya siku sita—kwamba wasite utendaji wao na kutambua wema wa Mungu wao, uhitaji wao kuu wa Mungu, na zawadi yake ya utulivu. 

Kwa kupumzika, tunakiri uaminifu wa Mungu: kwamba hata tunapoacha kufanya kazi, Mungu anaendelea kushikanisha ulimwengu wetu pamoja. 

Mwaka huu ninakualika, kama Bwana wetu na Mwokozi wetu alivyoalika wafuasi wake, kujitenga na kuenda kwake kupumzika kidogo, kupunguza mwendo na kugundua tena ajabu na furaha ya msimu wa Krismasi katika desturi upendazo za likizo hii. 

Lakini inakaa aje? 

Kwa siku nne zifuatazo, tutafanya mazoezi ya ibada ya pumziko: kumbuka wema wake, dhihirisha uhitaji wako, tafuta utulivu wake, na tumainia uaminifu wake. 

Utaitikia wito wake msimu huu wa Krismasi? Jitenge kwa muda mfupi, na pumzika. 

Ombi: Ee Bwana, unanijua vyema. Unajua kuwa ninatamani kufurahia msimu huu na familia na marafiki, lakini ninachukua mambo mengi na kusema kuwa nitayafanya ilhali siyawezi na kuguswa kupindukia maji yakizidi unga, na mwishowe, kuna wasiwasi na machungu mengi. Sitaki hayo yote mwaka huu. Kwa hivyo naja kwako na mikono wazi na moyo wazi. Niko hapa. Nifunze kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi wetu katika mahali pa pumziko. Geuza moyo wangu kustajabia urembo wako na kuimba sifa zako. Amina.

Unataka zaidi? Pakua kifungu chaKufungua Majina ya Yesu(Unwrapping the Names of Jesus) na utapokea shajara ya maombi ya Majina ya Yesu (Names of Jesus), Alamisho ya Kitabu ya Maombi ya Pumziko(Rest), na Ombi la Pumziko la Krismasi (Prayer for Christmas Rest) unaoweza kuchapishwa.  

 

siku 2

Kuhusu Mpango huu

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda.  Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo kutoka Biblia kuhusu Ujio (Unwrapping the Names of Jesus: An Advent Devotional) na utakuongoza kupokea pumziko la Yesu Krismasi huu kwa kuchukua muda kukumbuka wema wake, kudhihirisha uhitaji wako, kutafuta utulivu wake, na kutumainia uaminifu wake.

More

Tungependa kushukuru Moody Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://onethingalone.com/advent