Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii Mfano
Siku ya Nne: Tafuta Utulivu Wake
Umewahi kuhisi Roho Mtakatifu akikushawishi uchukue pumziko kutoka maandalizi ya likizo na uketi tu kidogo katika uwepo wa Yesu, lakini unampuuza na kuendelea na maandalizi yako?
Najua nimefanya hivyo.
Mara nyingi tunajisukuma kutia bidii, kuamka mapema na kulala usiku wa manane, kutumia kila saa tunao mchana. Halafu tunachoka sana na juhudi zetu, hatuwezi kufurahia msimu huo.
Na wakati mwingine, hii bidii ni barakoa ya kuficha machungu makuu ya ndani. Ikiwa tutajishughulisha na mambo mengi, ili tusifikirie kuhusu maumivu tunaobeba. Tunaogopa utulivu, kwa hivyo tunahakikisha tumefanya kila kitu, hata kama mtindo huu unatuumiza.
Si kwamba tunafaa kuwacha desturi na tamduni zetu na kutosheherekea Krismasi. Badala yake, lazima tuongeze nyakati za utulivu hata kati ya shughuli zetu zote ili tufanye kazi kutoka mahali pa uzima na pumziko. Ukweli ni kwamba wokozi wa Mungu unatujia tunapotubu na kupumzika, nguvu yake tunaponyamaza na kumwamini.
Msimu huu wa Krismasi, thubutu kuwa mtulivu, hata kama ni kwa dakika mbili pekee kila siku. Leta orodha yako ya kazi kwa Bwana na umwekee miguuni pake. Furahia uzuri wa uwepo wake unapotafakari majina yake na kumruhusu kuponya hayo machungu makuu.
Tangaza kwamba yeye ni Bwana wa maisha yako; dhihirisha uhitaji wako mkuu kwake, na ujiruhusu kuwa mtulivu. Furahi katika uwepo wake.
Yeye ni Immanueli—Mungu aliye nasi. Anaona. Anajua. Anasikia. Muache akutulize na upendo wake.
Sala: Tuliza moyo wangu na upendo wako, Bwana. Amuru amani maishani mwangu kama vile ulivyoamuru utulivu kwa dhoruba. Leta uponyaji na urejesho kwa uchungu ulio moyoni mwangu unaotokana na kupoteza mpenzi, kupitia janga ama kiwewe, matumaini kukatizwa na ndoto kuangamizwa. Wewe, uliye Ufufuo na Uhai, leta uhai upya katika hizi sehemu za roho yangu zilizokufa. Nipe tumaini mpya ya siku zijazo. Nifunze kuwa mtulivu na kupokea uwepo wako ambao unanipa uhai. Amina.
Kuhusu Mpango huu
‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda. Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo kutoka Biblia kuhusu Ujio (Unwrapping the Names of Jesus: An Advent Devotional) na utakuongoza kupokea pumziko la Yesu Krismasi huu kwa kuchukua muda kukumbuka wema wake, kudhihirisha uhitaji wako, kutafuta utulivu wake, na kutumainia uaminifu wake.
More