Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii Mfano

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

SIKU 3 YA 5

Siku ya Tatu: Dhihirisha Uhitaji Wako: 

“Asante, lakini ninajiweza.”

Umewahi kukataa kusaidiwa, hata kama unahitaji msaada? 

Wakati mwingine ni ngumu kukiri kwamba hatuwezi kufanya kila kitu wenyewe. Katika maandalizi ya Krismasi, hii inaweza kuleta uchovu na hasira. Lakini mwelekeo huo huo wa kujiweza ni hatari sana kwa maisha yetu ya kiroho. 

Ukweli ni kwamba tunahitaji Yesu. Lakini mara nyingi tunaishi kana kwamba tunajiweza peke yetu. Si mpaka tunachukua muda kutafakari kuhusu uzuri wa Mungu—utakatifu wake, upendo na ukarimu wake, sadaka yake ya ukombozi—ndipo tunatambua uhitaji wetu mkuu. Kuna unyonge unaotokana na kukiri uhitaji wetu, Yesu anaahidi kwamba walio maskini rohoni, walio wapole moyoni, na wanaotamani kufanya atakavyo Mungu, wanatuzwa na zaidi na zaidi ya Mungu mwenyewe. 

Kumbe kudhihirisha uhitaji wetu ni njia ya pekee ya kupokea utajiri kuu wa Kristo ambao Mungu ametuanadalia. 

Mtunga Zaburi anawaita watu wa Mungu kuabudu, kusujudu, na kupiga magoti mbele ya Muumba wao. Neno la Kiebrania la kuabudu lina maana la kusujudu. Kimwili ina maana ya kupiga magoti kwa utambuzi wa Ubwana wa Yesu; kiroho, ina maana ya kujisalimisha kwake.

Mwelekeo wetu kugeuzwa hivyo na vitu tunavyovipa kipaumbele pia kugeuzwa inawezekana iwapo kwanza tutachukua muda kutambua ukuu wa Mungu; ibada inatupeleka katika maono bora ya Mungu, unaotupeleka kwa maungamo na toba.  

Yesu anaonyesha hivi anapojiita Mzabibu, na wafuasi wake matawi. “Hamwezi kufanya chochote msipokaa ndani yangu,” anawaambia. “Lakini ukibaki ndani yangu […] utazaa matunda mengi.” Hata hivyo, Yesu hatuiti tutie bidii ili tuzae matunda mengi zaidi; bali, anatuita tukae ndani yake, tumngojee. Wanaoendelea kukaa ndani yake watazaa matunda mengi bila jitihada, kwani ni Roho yake inayozaa matunda hayo. 

Ruhusu uhitaji wako wa Yesu ukuletee pumziko na utulivu Krismasi huu. Hakuna shinikizo. Si lazima ufanye kila kitu pekee yako. Kwa kweli, unahitaji kupumzika. 

Maswali ya Kutafakari: Ni vipi ambavyo picha ya Yesu kuwa Mzabibu inakuathiri? Ni majina yapi mengine ya Yesu yanakuwezesha kutambua uhitaji wako? Ni njia gani utatumia kudhihirisha uhitaji wako na kupumzika kwa yeye leo? 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda.  Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo kutoka Biblia kuhusu Ujio (Unwrapping the Names of Jesus: An Advent Devotional) na utakuongoza kupokea pumziko la Yesu Krismasi huu kwa kuchukua muda kukumbuka wema wake, kudhihirisha uhitaji wako, kutafuta utulivu wake, na kutumainia uaminifu wake.

More

Tungependa kushukuru Moody Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://onethingalone.com/advent