Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano
Sisi wote tunataka watoto wana tabia nzuri, siyo? Wakati mwingine, tunamaaanisha tunataka watoto wetu waonekane wana tabia nzuri kwa wengine. Inaweza kumaanisha hawana mzaha ama hawana hamaki, ama unaweza kumaaanisha wanasema "tafadhali" na "asante" wakati unaofaa. Sasa kwa sababu watoto wangu wankua, nimeanza kufikiria kama kazi niliyofanya inafanya wang'ae nje ama inafanya wakue wazuri ndani mwao.
Miaka miwili ijayo, msichana wangu mwenye unri mkubwa ataenda chuo kikuu. Nachukia kukubali, lakini sitakuwepo kuhakikisha kwamba anaendelea vizuri. Kwa hivyo, nafanya kile ninachoweza sahii kuhakikisha atasikia sauti yangu kichwani mwake, nyakati hizo anapopambana na kufanya jambo linalofaa. Zuri zaidi ni, kama askie sauti ya Mungu? Kwa sababu Atakuwapo kila wakati-hata kama mimi sitaweza kuwa hapo.
Njia nzuri mno ya kufanya watoto wetu wajue sauti ya Mungu ni kuwafunza neno la Mungu, lakini kuwakariria maneno hayo -ama kuwafunza kulikariri-haitoshi. Ukitaka kuona watoto wako wakibadilishwa na nguvu ya neno la Mungu, basi lazima waone neno hilo likafanya kazi kwako-ikibadilisha mwendo wa maisha yako na uamuzi wako kila siku. Zungumza kuhusu neno kwenye meza pale sebuleni. Zungumza mkiwa ndani ya gari. Zungumza mkiwa na mazungumzo yasiyo rasmi na wengine. Saidia watoto wetu waone kwa makini jinsi neno la Mungu linabadilisha maisha yako yote.
Wakati huo huo, saidia watoto wako wajue Biblia kivyao kama kocha. Ni muhimu wajifunze kusoma Biblia na wamskize Roho Mtakatifu kivyao. Wasaidie kuchagua Mpango wa Biblia, na fuatilia na maswali. Haya ni mapendekezo ambayo unaweza kutumia kuanzisha mazungumzo kuhusu Biblia:
- Ni jambo lipi zuri zaidi umesoma katika Biblia wiki hii?
- Ni nini umesoma ambalo hukulielewa?
- Ni nini umesoma ambalo ungependa kujua zaidi?
- Ni nini Mungu anakuambia kupitia kile umesoma?
- Ni jambo lipi moja ambalo unaweza kubadilisha maishani mwako kupitia ulichokisoma?
Kama wazazi, tunafanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu kufunza watoto wetu kuhusu Mungu na ufalme wake. Muamini kwamba atamaliza kubadilisha watoto wako. Anawapenda kuliko tunavyoweza kuwapenda
Michael Martin
Msanidi wa programu wa Wavuti wa YouVersion
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe.
More