Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano
Ni mdogo katika mabinti wawili wa familia yetu, kwa hiyo utoto wangu ulijawa na wanasesele, michezo ya kupika pika na mingine- wote tuliwa watulivu, wenye nidhamu na michezo usalama. Sasa nikiwa kama mamam na watoto wawili wa kiume chini ya miaka mitano, nyumba yangu inaonekana na kusikika kama ilivyokuwa wakati wa utoto wangu. Kuombea watoto wangu imekuwa ni sehemu ya lazima katika safari ya umama, sana sana kwa sababu ya nguvu ya watoto hawa. Kama mama mkwe alivyonionya kuhusu maisha na watoto wa kiume, mwishowe nitawajua hata wauguzi wa huduma ya dharura kwa majina yao ya kwanza!
Sidhani kama niliwahi kufikiria kwamba miaka michache katika safari hii ningeweza kuona kuangukia uso kwa mtoto wangu mkubwa (kupelekea kuumia mzizi wa jino) na baadaye, mwaka mmoja baadaye, akiangukia kichwa (na kushonwa nyuzi tatu). Na sikuweza kufikiria mwanangu wa miezi kumi akipasuliwa kwa tatizo alilozaliwa nano. Kila hali imekuwa nje ya uwezo wangu. Kulikuwa hakuna nachoweza kuzuia kutokea- kitu kilichonifanya kupiga magoti na kuwaombea watoto wangu.
Kama mzazi, watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kuwalea, kuwalinda, kuwaonesha upendo na neema ya Yesu, na kuwaanda kwa safari yao ya maisha. Si mazingira yao ya kila siku au mueleko mzima wa maisha yao ni mambo tunayopaswa kuamua- au kuweza kuyadhibiti. Kwa hiyo kama wazazi tunatakiwa kufanya nini mwisho wa siku, wakati tumetumia nguvu zetu zote katika kuwalea, kwa heshima, katika kumcha Mungu na kuwaweka salama na wenye afya? Tunaweza kuondoa hofu zetu, mashaka yetu, na matarajio yasiyotimia kwa Mungu-tukishukuru kwa tunachofanya siyo tunayoongoza.
Tusichoke katika kuwaombea watoto wetu na kuwashika kwa mikono iliyo wazi kwa imani na tumaini kwa muumba wetu- anayewapenda watoto zaidi ya tunavyoweza na akiwashikilia katika mikono yake yenye nguvu.
Lisa Gray
YouVersion Localization Manager
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe.
More