Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano
Tulining'iniza mstari huu chumbani kwa mtoto wetu kabla hatujamleta kutoka hospitali, na tunauona kila usiku tunapomlaza. Ni kumbukumbu nzuri ya wito na wajibu ambao Mungu ameuweka kwetu kama wazazi wake.
Kama wazazi, tuna wajibu wa msingi kujenga msingi wa imani ya watoto wetu. Ikiwa tunapenda ama la, tunachora picha ya imani kwa watoto wetu kila siku. Kila neno, kila tendo, na kila jibu ni kama brashi ya kupakia rangi. Kuchora picha sahihi inaweza kuonekana ni ya kutisha katika maisha ya kila siku ya malezi. Ikiwa uko katikati ya kukosa usingizi usiku ukiwa na mtoto, ukihimili changamoto za kumfundisha kujisaidia, kuangalia masomo yake ya nyumbani na kazi za shule, au kuzungusha funguo za gari, malezi ni kazi ngumu. Lazima tuumbuke kwamba Mungu hatutarajii kufanya hili peke yetu, -anawapenda watoto wetu kuliko tunavyowapenda.
1. Omba pamoja na kwa ajili ya watoto. Kila siku.Kujenga msingi wa imani kwa watoto wako, maombi thabiti ni muhimu. Omba pamoja na kwa ajili ya watoto. Kila siku. Usiache kuomba kwa ajili ya watoto wako. Usiruhusu mazingira yao yafunike nguvu za Mungu. Hata kama sasa hivi mtoto wako anakimbia mbali na Mungu, ni kuwaombea tuu. Maombi yanaweza kubadilisha kila kitu.
2. Usifanye mwenyewe Wanasema kulea mtoto inahitaji kijiji. Unahitaji watu katika maisha yako kusaidia kuwaelekeza watoto wako katika njia sahihi. Hudhuria ibada kama familia. Tumika kanisani kama familia. Jiunge na kundi dogo unaloweza kujifunza nyakati zote za malezi. Wote tunahitaji jamii, na ni muhimu kwako na kwa watoto wako kuwa na imara, katika mahusiano ya kiimani.
Hujachelewa kuanza kuwekeza katika imani ya watoto wako. Na pia hujawahi sana kuanza. Anza safari ya imani kwa watoto wako na uanze kuwaelekeza kwa Mungu sasa.
Todd Dobberstein
YouVersion Product Manager
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe.
More