Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano
Uzazi ni ngumu, kusema kweli. Ni rahisi kwetu kukumbuka tukilea watoto wetu wanapokua-jinsi walivyo wadogo na walivyopendeza kisura, lakini ni ngumu zaidi kukumbuka jinsi walivyokua baraka alasiri ya Jumanne flani walipokua wakipiga makelele katika kona maalu, ama ulipobadilisha nepi ya elfu ya siku!
Lakini, kupitia mfadhaiko kutokana na uzazi, 1 Wathesalonike 5:16-18 inaweza kutusaidia kutizama kwa makini na macho mapya tunapopitia muda huu wa wazimu.
Kuwa na furaha kila wakati
Usipoteze matumaini nyakati hizo ngumu. Kumbuka kwamba kuwa mzazi ni mwito wenye thamani na uadilifu, ni faida kubwa Mungu ametupea, na ambayo utaona matunda siku moja, hata kama leo huhisi hivyo. Kumbatia ukweli kwamba Mungu ametupea heshima hii.
Usiwahi Sita Kuomba
Hakuna kitu watoto wetu wanahitaji kuliko Yesu Kristo ndani ya maisha yao. Kwa hivyo, jambo la muhimu zaidi tunaweza kufanya kama wazazi ni kuosha watoto wetu kwa maombi. 1Wathesalonike 5:17 inatuambia tusisite kuomba siku nzima-hata kama unahisi kama maisha yanavingirika kwa kasi mno.
Kuwa na Shukran
Kuwa na shukran kwa watoto wetu ni rahisi siku nyingine na ngumu zaidi siku nyingne. Lakini katika siku hizo ngumu, kumbuka kwamba hauko pekee yako. Unapohisi uchovu, huo ni mmojawapo wa nyakati nzuri kuelekea kwa Mungu kwa maombi. Mwuliza akupee furaha kwa upya, na umpee shukran kwa watoto wako. Anaweza na atakupea nguvu, furaha na shukran unayohitaji. Na ukijifunza kumegemea Mungu katika siku zako ngumu za uzazi, hatuna budi ila kumshukuru Mungu kwa kutupa watoto wetu!
Casey Case
Kiongozi wa Usaidizi wa YouVersion
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe.
More