Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Wanadamu wa vizazi vyote watakusanyika mbele za Bwana Yesu siku ya mwisho. Hapo kila mmoja atapokea hukumu yake kutokana na alivyoenenda duniani. Yesu anatuonyesha kuwa matendo ya watu walivyoenenda kwa usahihi mbele za Mungu yatakuwa yanakumbukwa hata kama wao walioyatenda watakuwa hawayakumbuki. Watapata heshima kubwa kwa sababu ya hayo. Kumbuka, hatuingii mbinguni kwa matendo mema. Wokovu ni zawadi ya Mungu kwa waaminio wote. Matendo mema ni wajibu wetu kuyatenda tukiwaduniani.Maana tu kazi yake [Mungu], tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo(Efe 2:10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz