Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
Daudi anatiwa hofu kwa kuona nguvu ya dhambi, jinsi iwezavyo kumfanya mtu kuwa kipofu kwa njia ya kunena moyoni mwake.Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa. Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema. Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii(m.1-4). Hivyo dhambi yamzuia asizitumie akili zake ambazo humwambia haiwezekani kumficha Mungu hata mawazo yetu ya siri. Msaada kwa muumini katika hali hiyo ni kuzikumbuka fadhili za Mungu:Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni. Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama. Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako. Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru(m.5-9). Hiyo inampa Daudi moyo wa kumwomba Mungu fadhili zake hizo:Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako(m.10) na ulinzi wake dhidi ya waovu na kiburi chao:Mguu wa kiburi usinikaribie, Wala mkono wa wasio haki usinifukuze. Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama(m.11-12). Tumkimbilie Mungu katika hali zote, maana kwake yatoka nuru ya kweli, nakatika nuru yake tutaona nuru(m.9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz