Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili ni niniMfano

Injili ni nini

SIKU 2 YA 3

Habari mbaya: Binadamu wote wamemkosea na gadhabu ya Mungu ipo juu yao.

Je, shida yetu kuu kama binadamu ni ipi? Wengi watasema kuwa umaskini, ungonjwa na uongozi mbaya ndizo shida zetu kuu. Lakini Biblia inatuambia ya kwamba shida yetu kuu ni dhambi. Dhambi ndio shida yetu kuu na inakumba kila mmoja wetu, kote duniani, sio Wakenya peke yake. Watu wa makabila yote wanakumbwa na hii shida ya dhambi na wamemuasi Mungu. Huu ndio ushuhuda wa Mungu kuhusu binadamu wote kote duniani:

Tazama, maandiko yanatuonyesha ya kwamba, hakuna hata mtu mmkoja ambaye ni mwenye haki mbele zake Bwana, hamna hata mmoja ambaye anayetenda mema mbele za Mungu, wote wamepotoka, wote wamekosa mbele za Mungu, na wote hawana thamani mbele zake Mungu. Huu ni ushuhuda wa kusikitisha sana kuhusu binadamu wote ulimwenguni.

Hata la kutia hofu zaidi ni, hamna mtu yeyote ambaye anaweza sema kwa hakika kuwa yeye hana dhambi maana Biblia inasema wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Sisi sote tumetenda dhambi, tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, wakubwa kwa wadogo, wote ni wenye dhambi. Watu wa makabila yote wametenda dhambi na wamepungukiwa na utukufu wa Mungu. Haijalishi hata kama ulizaliwa katika familia ya Kikristo ama wewe hufanyi zile dhambi kubwa kubwa, sisi wote tumetenda dhambi na tumepungukiwa na utufuku wa Mungu.

Kwa sababu tumemkosea Mungu, basi gadhabu yake ipo juu yetu maana mshahara wa dhambi ni mauti. Sisi wote hatuna thamani yeyote mbele zake Mungu, tumemkosea, kile ambacho tunastahili ni kifo, hukumu ya Mungu. Hakuna kitu ambacho tunaweza kufanya ili hukumu ya Mungu iweze kuondoka kutoka kwetu. Kwa nguvu zetu hatuwezi jiokoa kutokana na hukumu ya Mungu.

Je, unaielewa hii Habari mbaya inayowakumba binadamu wote duniani? Ni muhimu tuelewe kuwa sisi wote, wakubwa kwa wadogo, tumetenda dhambi na tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Na kwa sababu tumemkosea Mungu, hukumu yake ipo juu yetu, na hakuna kitu chochote tutafanya ili Mungu aweze kutusamehe. Tukielewa hay abasi itatusaidia kuona umuhimu wa injili, Habari njema ya wokovu kutoka kwa Mungu.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Injili ni nini

Nini kinakujia akilini unapoisikia neno "Injili"? Kwa urahisi, Injili ni habari njema kuhusu Yesu—yeye ni nani, alichofanya kutuokoa kutoka kwa dhambi, na jinsi hilo linavyobadilisha kila kitu. Hii ni habari muhimu zaidi utakayosikia au kushiriki. Kuna Injili moja ya kweli, na ni muhimu kuielewa vyema, kwani kuna “injili” nyingi zilizopotoka ambazo haziwezi kutuongoza kwa Mwokozi.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/