Injili ni niniMfano
Injili ni nini?
Je, injili ni nini? Kwa njia inayoeleweka zaidi, injili ni Habari njema kumhusu Yesu Kristo na yale ambayo ameyafanya ili kuwaokoa wanadamu kutokana na dhambi. Hivyo hii Habari ya uokovu ndio Habari njema kabisa duniani na inatubidi tuifahamu vizuri. Maana kunazo Habari mingi za injili ambazo sio sahihi na zinapotosha wakristo wengi. Tutaangazia maandiko ili tuweze kuelewa kwa kina injili ya kweli ni ipi, tuweze kuelewa jinsi ya kipekee tutaweza okolewa kutokana na dhambi, na tujue jinsi ya kupokea huu uokovu.
Kwanza, injili ni Habari njema ya Mungu. Mungu ndiye mwanzilishi wa injili. Injili haijatokana na binadamu yeyote ama kanisa lolote. Injili ni Habari njema kutoka kwa Mungu ambaye ni muumba wa mbingu na nchi. Hata ingawa kuna wale wanasema kuwa injili imetokana na wazungu, tunaweza kuona hapa kuwa injili ni Habari njema ambayo imetoka kwa Mung una sio kwa yeyote. Mungu ndiye mwanzilishi na ameinena hii Habari njema ya uokovu kwenye maandiko.
Pili, Habari hii njema ni kuhusu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Injili inamhusu Yesu Kristo ambaye alikufa msalabani kwa ajili ya wenye dhambi.
Tatu, injili ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini. Ni kwa kupitia injili pekee wenye dhambi wanapata msamaha wa dhambi zao na kupatanishwa na Mungu. Hamna nguvu nyingine ya kuwaokoa wenye dhambi ila tu kupitia kwa injili.
Injili ni Habari njema ambayo huokoa na kubadilisha Maisha ya binadamu. Ndio suluhu pekee kwa shida yetu kuu ambayo ni dhambi. Hivyo ni vizuri tuijue na kuifahamu vizuri Habari hii njema ya wokovu. Ili tuweze kuilewa vizuri Habari hii njema ya wokovu, tutaanza kwa kuelewa Habari mbaya ambayo inawakumba binadamu wote, tuweze kuona suluhu ya injili na jinsi amabayo tunafaa kupokea huu wokovu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Nini kinakujia akilini unapoisikia neno "Injili"? Kwa urahisi, Injili ni habari njema kuhusu Yesu—yeye ni nani, alichofanya kutuokoa kutoka kwa dhambi, na jinsi hilo linavyobadilisha kila kitu. Hii ni habari muhimu zaidi utakayosikia au kushiriki. Kuna Injili moja ya kweli, na ni muhimu kuielewa vyema, kwani kuna “injili” nyingi zilizopotoka ambazo haziwezi kutuongoza kwa Mwokozi.
More
Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/