Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili ni niniMfano

Injili ni nini

SIKU 3 YA 3

Habari Njema: Kuna msamaha wa dhambi ndani ya Kristo.

Wote wametenda dhambi na hukumu yake Mungu ipo juu yao, je, kuna tumaini lolote kwa wenye dhambi? Habari njema ni kuwa kunayo njia ambapo wenye dhambi wanaweza kusamhewa dhambi zao na kupatanishwa na Mungu. Na njia pekee kwa wenye dhambi kusamehe ni kupitia tu kwa Yesu Kristo. Hii inawezekana tu kwa sababu Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya wenye dhambi. Kwa kifo chake msalabani Yesu alilipa deni yote ya dhambi. Hukumu ya Mungu ambayo iliokuwa juu ya binadamu Yesu aliichukuwa yote.

Sasa wenye dhambi wanachotakiwa kufanya ni kutubu na kumwamini Yesu Kristo kuwa alikufa kwa ajili ya dhambi zao ili waweze kusamehewa dhambi na kuunganishwa na Mungu. Ni vizuri tukumuke kwamba hatusamehewi dhambi kwa sababu ya matendo yetu mema, la, kwa matendo yetu mema hamna yeyote ambaye anaweza kuokolewa. Mungu hatukoi kwa sababu sis ni watu wazuri, la hasha, sisi wote tumekosa na hatuna thamani yeyote mbele zake Mungu. Ni kwa neema tu Mungu anatuokoa kutoka kwa dhambi zetu. Hivyo tusije tukajipiga kifua na kuringa kwa wokovu wetu. Hatukuchangia chochote kwa uokovu wetu. Uokovu wetu ni kazi ya Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho. Kitu ambacho tumechangia ni dhambi zetu ambazo zilifanya Yesu akasulubiwe. Hivo tujue kuwa uokovu wetu ni kibali kwetu kutoka kwa Mungu ambao tumeipokea kwa Imani.

Na huu uokovu ambao Yesu ametufanyia ni wa watu wote bora tu wamwamini. Haijalishi wewe ni kabila gani ama kama wewe dhambi zako ni mingi, maana kila mtu atakayeliita Jina la Bwana, ataokolewa. Je, wewe umefahamu hii Habari njema kuwa kuna msamaha wa dhambi ndani ya Kristo? Njoo hii leo kwa Yesui li uweze kuokolewa kutoka kwa dhambi na upatanishwe na Mungu.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Injili ni nini

Nini kinakujia akilini unapoisikia neno "Injili"? Kwa urahisi, Injili ni habari njema kuhusu Yesu—yeye ni nani, alichofanya kutuokoa kutoka kwa dhambi, na jinsi hilo linavyobadilisha kila kitu. Hii ni habari muhimu zaidi utakayosikia au kushiriki. Kuna Injili moja ya kweli, na ni muhimu kuielewa vyema, kwani kuna “injili” nyingi zilizopotoka ambazo haziwezi kutuongoza kwa Mwokozi.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/