Uaminifu, Tunda la RohoMfano
Uaminifu dhidi ya kuzuia
Hadithi ya Biblia: Ibrahimu na Isaka Mwanzo 22: 1-18
Kifungu cha Mada: Waebrania 11:6
Katika Biblia nzima, Mungu anaonyesha sehemu muhimu ya imani na uaminifu ni kukubali na sio kuzuia mambo kutoka kwake. Hiyo ndio sababu wiki hii tunapigana na dhambi ya kuzuia. Kuzuia jambo ni kukataa kupeana jambo ambalo linatakikana. Inaweza pia kumaanisha kukandamiza au kushikilia.
Katika hadithi ya Biblia ya leo, Mungu aliuliza Ibrahimu jambo KUBWA! Yeye angechagua kuizuia kutoka kwa Mungu au kuwa tayari kumtii. Kwa maisha kubwa ya Ibrahimu, yeye na mke wake Sarah hawajaweza kuwa na watoto. Mungu aliahidi Ibrahimu na Sara watoto (watoto, wajukuu, nk) wengi kama nyota za angani. Kwa hiyo, ni jambo la kushangaza kwamba walikuwa bado hata kupata mtoto 1.
Kisha siku moja ya kimiujiza, Mungu akafunguwa tumbo la Sara, naye akapata mimba, hata ingawa alikuwa mzee sana! Akawa na mtoto aliyeitwa Isaka, na wakampenda na kumlea. Mungu akaamua kupima Ibrahimu ili kuona kama alikuwa tayari, au kama angeweza kuzuia kutoka kwa Mungu. Mungu akamwita Ibrahimu na kumwambia achukue Isaka mwanawe juu ya mlima, na kumchinja yeye kama sadaka ya kuteketezwa. Asubuhi hiyo, Ibrahimu akaondoka, akatandika punda wake. Akachukua watumishi wawili na Isaka mwanawe, na vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya dhabihu. Wakasafiri hadi sehemu ambaye Mungu alisema, kisha Ibrahimu na mwanawe wakaendelea, wakajitayarisha kwa ajili ya sadaka.
Isaka akamwambia baba yake, "moto na kuni ni hapa, lakini yuko wapi mwana-kondoo wa dhabihu?" Ibrahimu lazima alikuwa na hofu kwa kweli kumtii Mungu! Lakini aliamini Mungu na kuendelea na mpango. Wakatengeneza madhabahu, na Ibrahimu akaweka Isaka juu yake. Hata hivyo, wakati Ibrahimu anainua kisu, Mungu akamsimamisha! Mungu akamwambia Ibrahimu asiumize mvulana na akasema, "Sasa najua ya kuwa unamcha Mungu, kwa sababu hukuzuia mwanao, mwanao wa pekee." (Mwanzo 22:12)
Mstari hii inaonyesha kwamba Mungu alikuwa anapima Ibrahimu ili kuona kama angeweza kuizuia chochote kutoka kwa Mungu. Tunaweza kusherehekea pamoja na Ibrahimu kuwa yeye alipita mtihani! Ibrahimu alijionyesha kuwa tayari, na hakushikilia kitu chochote. Mungu pia atatupa mtihani. Yeye anaangalia wanaume na wanawake, wavulana na wasichana ambao watakuwa tayari kutoa kwa Mungu chochote atauliza. Mungu anatafuta wale ambao hawawezi kuzuia kutoka kwake. Je, uko tayari kumtii Mungu? Je, unaweza kupita mtihani mgumu?
Maswali:
1. Je, Umewahi ficha habari, urafiki, au wema kutoka kwa mtu? Wakati gani na kwa nani?
2. Kama Mungu angekuuliza kutoa kitu yako muhimu katika maisha, ingekuwa nini?
3. Je, Mungu amewahi kukupima?
Maombi kwa maisha:
Je, kuna kitu ambacho Mungu anakuuliza kuachana naye wiki hii? Chukua muda kufikiria ni nini hio, na kisha kuomba kwamba Mungu akupe nguvu kuachana kwa muda. Inaweza kuwa chai, Facebook, au chakula unaependa. Ili kushinda vita hii, chagua kuachana na jambo hilo wiki mzima.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa kusoma wa siku saba unaonyesha vita vya UAMINIFU dhidi ya kuabudu sanamu, ukosefu wa uaminifu, kusitasita, kutoaminika, shaka, uasi na kunyima. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UAMINIFU katika maisha yetu ya kila siku.
More
Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/champions/