Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uaminifu, Tunda la RohoMfano

Uaminifu, Tunda la Roho

SIKU 2 YA 7

Uaminifu dhidi ya Uhaini

Hadithi ya Biblia: Shadraka, Meshack na Abednego - Danieli 3: 1-21

Kifungu cha Mada: Zaburi 86:11

Pambano letu wiki hii ni uaminifu dhidi ya uhaini. Ni muhimu

sana kwa Mungu kwamba sisi ni waaminifu kwake, na ni sehemu kubwa ya kuwa Mkristo mwaminifu. Uaminifu ina mengi ya kufanya kwa imani pia. Wakati tuko waaminifu kwa marafiki shuleni, ina maana wanaweza kutuamini sisi kuweka siri zao, kusimama kwa ajili yao, na daima kuwa kwa upande wao, ikiwa wapo au la.

Ugumu inakuja wakati tunakumbana na shinikizo la marafiki. Tunahisi shinikizo la marafiki wakati wengine wanatusukuma kubadili mienendo yetu, maadili au tabia kuandamana na kikundi. Inaweza kuwa vigumu sana kusimama imara katika uaminifu wetu kwa Mungu wakati tunakabiliwa na shinikizo la wengine kutoka shuleni au katika majirani. Wao wanaweza taka tusiwe na huruma na mtu mwingine, au wanaweza taka sisi kusema tunaamini katika miungu mingine wakati hatufanyi hivyo. Uaminifu kwa Mungu inamaana kwamba yeye anaweza tumainia sis, bila kujali shinikizo karibu nasi. Ina maana kwamba sisi ni wa Mungu bila kujali hali. Wakati tuko waaminifu, hakuna chochote watu watasema itafanya sisi kukana Yesu Kristo au Mungu shuleni, mchezoni, au kwa majirani.

Katika hadithi ya leo ya Biblia, tunaona Shadraka, Meshaki, na Abednego wanapata shinikizo la kuinamia sanamu ya dhahabu, mfalme aliyoisimamisha. Ahadi hiyo ilitolewa kwamba mtu yeyote ambaye hawezi kumwinamia atatupwa katika tanuru la moto! lazima walipata shinikizo kubwa kutoka kwa kila mtu karibu nao. Lakini walichagua wasikubali shinikizo, hata kama ilimaanisha kifo.

Bila kujali kiasi cha onyo walipata na vitisho katika maisha yao, waliamua kuwa waaminifu kwa Mungu. Walikataa kukubaliana. Mfalme akakasirika sana na kuwarusha ndani ya tanuru! Tanuru ilikuwa moto hivi kwamba ikawaua watu waliorusha Shadraka Meshaki na Abednego.

Mfalme alishangazwa na kile alichokiona, kwa sababu, ingawa aliwatupa watu 3 pekee, sasa anaona watu 4 wakitembea wakiwa hai ndani ya tanuru! Mfalme akawaamuru watoke nje, na walipotoka, hakukuwa hata na harufu ya moto juu yao. Kuona hii, mfalme akamsifu Mungu wao, ambaye aliwaokoa kutokana na moto! Katika baadhi ya nchi, hata leo watu wanauawa wanapo sema hadharani kuwa Wakristo. Lakini kwa wale ambao wanaishi katika nchi zenye uhuru wa dini, bado inaweza kuwa vigumu hadharani kudai kuwa Mkristo kukiwa na shinikizo la marafiki. Ikiwa tutashinda vita hii ya uhaini, ni lazima tukubali kuwa waaminifu kwa Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo, bila kujali gharama.

Maswali:

1. Je, umewahi kumwambia siri ya rafiki yako kwa wengine?

2. Ni shinikizo gani ipo ili ufiche kwamba wewe ni Mkristo katika sehemu unaoishi?

3. Ikiwa rafiki hayupo, tunaweza kosa kuwa waaminifu, sababu hawaonekani?

Maombi kwa maisha:

Tafuta nafasi wiki hii kusema waziwazi shuleni au katika jamii kuwa wewe ni Mkristo, na kwamba unaamini Yesu Kristo. Baada ya hapo, furahia kwamba umekuwa mwaminifu na kikundi kidogo, licha ya shinikizo yoyote unakabili.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Uaminifu, Tunda la Roho

Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa kusoma wa siku saba unaonyesha vita vya UAMINIFU dhidi ya kuabudu sanamu, ukosefu wa uaminifu, kusitasita, kutoaminika, shaka, uasi na kunyima. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UAMINIFU katika maisha yetu ya kila siku.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/champions/