Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uaminifu, Tunda la RohoMfano

Uaminifu, Tunda la Roho

SIKU 4 YA 7

Uaminifu dhidi ya Kutotii

Hadithi ya Biblia: Wapelelezi katika kanaani Hesabu 13: 1-3,17-33, 14: 1- 11

Kifungu cha Mada: Hesabu 14:41

Kuwa mwaminifu ni pamoja na kuwa mtiifu. Hatuwezi kusema

"Mimi ni mwaminifu kwa Mungu" na wakati huo, tunakosa kutii amri zake. Hiyo ndio tunasoma wiki hii: mapambano ya "Kutotii" dhidi ya "Uaminifu". Kutotii mara nyingi inaonekana wakati tunafanya jambo hatupaswi kufanya. Kwa mfano, kama mama yako anasema kwamba huwezi kwenda nyumba ya rafiki yako kucheza leo, lakini wewe bado unaenda, unakosa utii. Alisema LA, lakini ukaasi na ukaenda. Watu wengi katika makanisa wana ufafanuzi huu kwa uasi. Kwa mfano, kama Wakristo wanaamini kuwa hawaruhusiwi kuvuta sigara, lakini bado wanafanya hivyo, hiyo ina maana wao ni wakaidi. Hii ni kweli. Kama tunaambiwa tusifanye kitu, na sisi tunafanya hivyo, tunakuwa waasi.

Kuna aina nyingine ya kuasi ambaye ni lazima pia kuangalia. Kama mama yako anakwambia uenda dukani kuchukua vitunguu kwa chakula cha jioni, na unakosa kwenda, hii pia ni uasi. Kama Mungu anatueleza kufanya jambo fulani, na tunakosa kufanya hivyo, tunakuwa wakaidi.

Hiki ndicho kilichotokea katika hadithi ya Biblia ya leo. Watu wa Israeli waliokolewa kutoka utumwa wao katika Misri, na kusafiri katika jangwa, upande wa nchi nzuri ambaye Mungu aliahidi. Walipofika karibu, Mungu akawasimamisha. Akauliza Musa kutuma viongozi 12, kama wapelelezi katika nchi ya ahadi. Hawa watu 12 walikwenda katika nchi na kupeleleza watu, miji, majengo, na mazao. Walikwenda ili kuona kama nchi ilikuwa nzuri au mbaya.

Hadi hatua hii, Waisraeli walikuwa walitii kila kitu ambacho Mungu aliwataka kufanya. Wakatuma wapelelezi 12 kama vile Mungu aliwaambia. Hata hivyo, wakati wapelelezi waliwasili nyumbani, wakakosa kukubaliana. Wote 12 walisema kuwa nchi ilikuwa kubwa, unatiririka maziwa na asali. Wakaja na rundo la zabibu kubwa kuonyesha watu kuhusu uwezekano wa kilimo. Lakini 10 wa wapelelezi wakasema kuwa watu walikuwa wakubwa mno na miji pia ni ngome, hivyo wanapaswa WASI ende kuchukua nchi. Wapelelezi 2 tu walisema hata ingawa watu walikuwa wakubwa, wanapaswa bado kwenda. Israeli yote ikasikiliza ripoti ya wapelelezi 10, na hawakutaka kwenda.

Mungu akawa na huzuni na kukasirika kwa sababu watu walikuwa wamevunjika mioyo. Walitaka kutomtii Mungu, kukataa kwenda katika nchi. Ni rahisi sana kwetu kuvunjika moyo na kuwa na huzuni tunapoona jambo lisilowezekana. Wakati mwingine habari kwenye TV inatuvunja moyo au maoni kutoka kwa watu wengine kutufanya tuwe na huzuni. Lakini Mungu anataka tuwe na imani kwake na kumwamini. Kama Mungu anatuambia tufanye jambo fulani, tunahitaji kuwa tayari kuchukua hatua ya imani na kumtii Mungu. Yoshua na Kalebu walikuwa wapelelezi wawili ambao waliamini Mungu, na kuwatia moyo watu kwamba ilikuwa inawezekana. Je, utakuwa kama Yoshua na Kalebu, tayari kutii Mungu, na kulinda moyo wako?

Maswali:

1. Ni lini mara ya mwisho umevunjika moyo na kuwa na huzuni moyoni wako? Jinsi gani umefarijika?

2. Je, Mungu amewai kukuuliza kufanya jambo ambalo ilionekana haiwezekani au ni vigumu sana?

3. Je, unajiona mwenyewe kama unatii Mungu?

Maombi kwa maisha:

kwanza iwe ni jambo Mungu alikuuliza USI fanye, na kingine Mungu alikuuliza ufanye. Mtii Mungu katika mambo yote mbili ili kushinda dhidi ya uasi.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Uaminifu, Tunda la Roho

Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa kusoma wa siku saba unaonyesha vita vya UAMINIFU dhidi ya kuabudu sanamu, ukosefu wa uaminifu, kusitasita, kutoaminika, shaka, uasi na kunyima. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UAMINIFU katika maisha yetu ya kila siku.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/champions/