Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uaminifu, Tunda la RohoMfano

Uaminifu, Tunda la Roho

SIKU 3 YA 7

Uaminifu dhidi ya Kusita

Hadithi ya Biblia: Bwana anamwita Samueli 1 Samweli 3: 1-21

Kifungu cha Mada: Waebrania 11:1

Pambano letu wiki hii ni uaminifu dhidi ya kusita. Ni muhimu sana sisi kuitikia Mungu, na ni sehemu kubwa ya kuwa Mkristo mwaminifu. Mungu anazungumza nasi kwa njia nyingi, lakini mara nyingi, hatutaki kutulia na kumsikiliza. Tunachagua kutulia na kusubiri kabla ya kujibu Mungu. Wakati mwingine hatuwezi toa jibu yeyote, tunafikiri kwamba Mungu hajui. Tunawezaje kujua kama ilikuwa ni Mungu anazungumza nasi? Je, umewahi jipata na mashaka kwamba Mungu kweli alikuwa anakuuliza ufanye kitu?

Hadithi ya Leo ya Biblia ni kuhusu kijana ambaye pia alikuwa na mashaka kwamba Mungu alikuwa anazungumza naye. Samweli alikuwa kijana mdogo ambaye alipewa Bwana na mama yake. Hata ingawa yeye bado alikuwa mdogo, Samweli aliishi katika hekalu, na kumtumikia Mungu na kuhani Eli. Usiku moja, walipokuwa wanakwenda kulala, Samweli akasikia mtu anamuita. Yeye akadhani ni kuhani Eli, hivyo aliamka na kwenda kwa kuhani. Hata hivyo, Eli akasema, "Mimi sijakuita, rudi ukalale." Hii ikafanyika mara mbili zaidi, na Eli akamwambia Samweli arudi akalale. Hata hivyo, kila wakati Samweli alikuwa na uhakika mtu alimwita! Kwa mara ya tatu, kuhani Eli akajua kwamba ni lazima ni Mungu anamuita Samweli. Akaagiza Samweli kujibu Mungu kwa kusema, "Nena, Bwana, kwa maana mtumishi wako anasikiliza."

Wakati Mungu alimwita Samweli, alikuwa tayari na akamuitikia Mungu kikamilifu! Kisha Mungu akatoa neno maalum kwa Samweli, na maisha yake kama nabii ikaanza, ingawa yeye bado mdogo. Si muhimu umri gani uko, au jinsi gani unajisikia kuharibika. Mungu anatafuta wavulana na wasichana ambao wataisikia sauti yake, na kuamini na kutii. Dhambi moja ambayo tunapambana ni majaribu ya kusita, kukosa kuamua au kusubiri kabla ya kujibu Mungu. Katika hali ya Samweli, hakuweza kujibu kwa usahihi mpaka mara ya 4, lakini hiyo ilikubalika kwa Mungu.

Kama unafikiri kuhusu hilo, Samweli bado aliitikia jioni hiyo hiyo. Hata hivyo, nini kitatokea kama Mungu anatuita kufanya kitu, na hatuwezi kujibu jioni hiyo hiyo? Na kama tunasubiri wiki ili kujibu Mungu? Labda Mungu atakuonyesha mtu katika shule ambaye anahitaji msaada. Je, utasita, au utajibu haraka?

Mstari yetu la kumbukumbu kwa leo inaonyesha kwamba kuwa na imani katika Mungu ambaye hatuwezi kumuona inaonyesha tuna imani. Kuamini kwamba amezungumza nasi, hata ingawa hatuwezi kumsikia kwa masikio yetu, ina maana tuna imani. Kama mimi na wewe tuta enda kuwa na imani yenye nguvu, ambayo inaweza kushinda mapambano, ni lazima kuamini wakati Mungu anazungumza nasi. Na kama kweli tunaamini, tutatenda bila kusita sana!

Maswali:

1. Ni wakati gani "kimya" inamaanisha jibu ni "hapana"?

2. Je, Mungu amewahi kukuuliza kufanya kitu? Jinsi gani ulijua ni Mungu?

3. Jinsi gani tunaweza kushinda shaka kwamba Mungu anatutaka sisi katika mji fulani, kazi, au urafiki?

Maombi kwa maisha:

Mwombe Mungu azungumze nawe wiki hii, na akuelekeze kufanya kitu fulani. Fanya mazoezi ya kutii mara moja bila kusita. Kama utasahau na kusubiri, uliza Mungu akupe zoezi jingine.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Uaminifu, Tunda la Roho

Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa kusoma wa siku saba unaonyesha vita vya UAMINIFU dhidi ya kuabudu sanamu, ukosefu wa uaminifu, kusitasita, kutoaminika, shaka, uasi na kunyima. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UAMINIFU katika maisha yetu ya kila siku.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/champions/