Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

SIKU 2 YA 30

Hosea aliitwa na Mungu awe nabii huko Israeli ya Kaskazini. Mungu anamtuma amwoe mke mzinzi. Huenda Gomeri alitokea kuwa mzinzi baada ya kuolewa tu, lakini hatuna uhakika. Mungu alimwagiza Hosea hivyo ili kuonyesha uhusiano uliopo kati yake na taifa la Israeli. Taifa hili linafanya uzinzi wa kiroho kwa kumwacha Mungu na kugeukia ibada za miungu. Mungu anadhihirisha hali yao hiyo kwa kumwambia Hosea,Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana(m.2). Jina la mtoto Yezreeli linatabiri juu ya hukumu ya Mungu kwa taifa hilo (m.4:Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli). Fikiria kwamba hata maisha ya kifamilia ya Hosea ni unabii kwetu.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/