Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona(m.38-39). Yesu anafundisha juu ya hali inayotokea mara kwa mara kwamba mtu katika kumfuata yeye hukabiliwa na uchaguzi mgumu sana. Maana akichagua kumfuata Yesu atavunja uhusiano wake mzuri na wazazi au ndugu, hata inawezekana watakuwa maadui zake. Huenda atajisikia kana kwamba anaipoteza nafsi yake. Lakini amchaguaye Yesu huiokoa nafsi yake milele!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/