Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi(m.11)?Swali hili liliulizwa na Mafarisayo walipoona Yesu ameketi nyumbani kwa Mathayo pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi. Baadaye huyu Mathayo akawa mtume, tena ndiye aliyeiandika Injili hii tusomayo. Yesu alijibu swali namna hii:Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi(m.12-13)! Yesu hakula nao ili kushirikiana nao katika maovu yao, bali kwa sababualiwapenda. Ni wenye thamani kubwa kwa Mungu. Alitaka awaokoe. Je, sisi Wakristo tunawapenda wasiomjua Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/