Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Ni maelezo juu ya maana ya tendo la ishara la Hosea katika ml.1. Uhusiano wa Mungu na Israeli ni kama ndoa iliyovunjika kwa sababu ya uzinzi wa “mama” (Ufalme wa Kaskazini). Uzinzi wake ni upi? Tafakari m.5 na 13 ambapo “wapenzi” ni mfano wa miungu:Mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu....Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema Bwana. Ilikuwa haki ya mke kupewa nguo na chakula na mume wake (Kut 21:10,Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia). Kwa sababu Israeli si mke wake tena, Mungu atamvua nguo zake na kuharibu mazao ya nchi yake. Ila angalia, Mungu anasema hivyo kwa sababu anawapenda Waisraeli na kutaka wamrudie. Inaonekana katika m.7 ilipoandikwa kuhusu Israeli, Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/