Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Wito wa Mungu kwa Hosea ni kuendelea kumpenda mke wake. Ndivyo Mungu anavyopenda watu wake waliomwasi. Ingawa Hosea amemkomboa tena Gomeri, hawatakaa pamoja kama mume na mke. Ni mfano wa kinabii jinsi Waisraeli watakavyokuwa na muda wa kukaa utumwani. Nchi za ugeni ni adhabu wanayoipata kwa kumwasi BWANA. Lakini pia ni nafasi ya kutafakari walimwacha nani. Hivyo upendo wa Mungu ni wenye nguvu na ushindi. Israeli watatubu, naye Mungu atawapokea. Je, wema wa Mungu katika Kristo umekuvuta upate kutubu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/