Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tumaini, Jibidishe, Na PumzikaMfano

Trust, Hustle, And Rest

SIKU 4 YA 4

Kupumzika

Kama tulivyoona katika siku chache zilizopita, kutumaini ni kugumu lakini ni tendo rahisi la kutambua kwamba hatuhusiki kuleta matokeo kupitia kazi zetu-- Mungu ndiye. Mara tutakapochukua hatua hii muhimu, ni wazi kwamba ni sahihi kujibidisha, kutumia vipawa alivyotupa Mungu kutimiza wito wetu. Lakini tunajuaje kama wote tunatumaini   na  kujibidisha? Kujibidisha ni rahisi kuonekana. Kunapatikana katika masanduku yetu ya barua pepe, orodha ya vitu vya kufanya, na mawazo yaliyojaa. Lakini tunajuaje kama kweli tunatumaini katika Mungu, kuliko wenyewe, kuleta matokeo? Yawezekana kiashiria kizuri ni kama tuko au hatuko kwenye pumziko.  

Pumziko ndilo wote tunalolitafuta. Haichukui muda kutambua kwamba kupumzika maana yake ni zaidi ya kutumia muda mwingi nje ya ofisi. Kukiwa na mstari uliofifia kati ya kazini na nyumbani, inaweza kuonekana haiwezekani kutenganisha kimwili na kiakili mahitaji ya uzalishaji usiotosha. Hata tunapokuwa nyumbani, tunaangalia barua pepe, instagram, kalenda, n.k. Siku zote tunafanya. Hatupumziki.  

Twawezaje kupata pumziko, ambalo wote tunalitamani sana? Mtakatifu Agostino anatoa majibu: " mioyo yetu haipumziki, mpaka itakapopata pumzko kwako." Hatutapumzika mpaka tutakapopumzika kwa Mungu peke yake. Hii inamaanisha kwamba wakati tunajibidisha, lazima tumtumaini Mungu ambaye, katika historia yote amekuwa mwaminifu kuwatunza watu wake. Kama tunaamini tabia ya Mungu, kulinda vizuri karama alizotupatia, tunaweza kupumzika kwa uhakika tukijua kwamba matokeo yako mikononi mwake, kwamba yeye anatawala na hutufanyia mema. Katika maneno ya Sulemani katika Mithali 16:33, " Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo, lakini kila hukumu zake zote ni za Bwana."

Hii ndiyo njia pekee kwenye ukweli na kupumzika kitabia, kiakili, na kiroho, na inaanza na kujisalimisha katika mpango wa Mungu wa Sabato. Kwa maneno ya Mchungaji Timothy Keller: “Tunatakiwa kuifikiria sabato kama kitendo cha imani. Mungu alichagua sabato kutukumbusha kwamba anafanya kazi na kupumzika. Kuifuata sabato ni njia ya kinidhamu na uaminifu kukumbuka kwamba wewe siye unayeufanya ulimwengu kuzunguka, kuhudumia familia yako, wala si wewe unayefanya miradi yako iendelee mbele.”

Kwa nini ni muhimu sana kutawala vizuri mvutano kati ya kuamini na kujibidisha? Kwa sababu mwisho wa siku, tunapotegemea juhudi zetu pasipo kumtumaini Mungu, tunajaribu kumdharau Mungu au kuiba utukufu wake, kitu kinachopelekea kutokuwa na amani. Mkristo, jipe moyo. Maagizo haya ya kibiblia hayapingani. Umeitwa kumwamini Mungu na kufanya kazi kwa bidii. Tutakapokubali mvutano huu, tunaweza kupumzika tukijua kwamba tuko kwenye ushirika mzuri na aliyetuita.

Kama umefurahia kusoma mpango huu, utapenda ibada zangu za kila juma, zitakusaidia zaidi kujiunga na injili kazini kwako. Jiandikishe hapa.

siku 3

Kuhusu Mpango huu

Trust, Hustle, And Rest

Biblia inatuagiza kufanya kazi kwa bidii, lakini pia inatuambia ni Mungu-- siyo sisi --anayetoa matunda ya kazi yetu. Kama mpango huu wa siku nne utakavyoonesha, taaluma ya kikristo lazima ikubali mvutano kati ya “kuamini” na “kujibidisha” ili kupata mapumziko halisi ya Sabato.

More

Tungependa kumshukuru Jordan Raynor kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.jordanraynor.com/trust/