Tumaini, Jibidishe, Na PumzikaMfano
Bidii
Katika siku chache zilizopita, tumekuwa tukiangalia mvutano ambao sisi wakristo inabidi kufanya katika kazi zetu, kati ya kumtumaini Mungu na bidii ili kufanya mambo yatokee katika kazi tuliyoichagua. Kama tulivyoona jana, Sulemani anaweza mfululizo kuongoza mawazo yetu juu ya somo hili, tukianzia na kukabidhi kazi zetu kwa Bwana (Mithali 16:3). Mstari wa tisa wa sura hiyo hiyo, Sulemani unatutaka tufanye bidii, akisema, "Moyo wa mtu hufikiria njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake."
Ndiyo, Mungu ametuita tumtumaini, lakini vilevile ametupa neema ya akili kupanga na kutekeleza. Tukizikabidhi kazi zetu kwa Bwana, tumeitwa kufanya bidii, kufanya "kwa moyo wetu wote, kama kufanya kwa Bwana" (Wakolosai 3:23).
Mara nyingi, ninaogopa kwamba wakristo hutazama sana kwenye ama kutumaini au kujibidisha. Wakristo wengine wanatumia "kumngoja Bwana" kama leseni ya uvivu usio wa kibiblia, wakati wengine wanajibidisha sana kwamba hawako vizuri kiafya, kiroho, na kihisia. Uzuri wa Mithali 16:9 ni kwamba unabadiki mvutano uliopo katika kweli hizi mbili. Ndiyo, lazima tutambue kwamba "Bwana huziongoza hatua zetu", lakini pia ni sahihi na vyema kwetu "kupanga njia zetu wenyewe", kubuni, kujenga, kuendeleza, kupaka rangi, kubuni, kuandika, kutangaza, na kuuza.
Kazi yetu ni moja ya njia za msingi katika kuwapenda majirani na kuutumikia ulimwengu. Kumbuka, kazi ilikuwepo hata kabla ya anguko katika Bustani ya Edeni. Kazi ni kitu chema cha ndani kilichobuniwa na Mungu kuonesha tabia yake na upendo na kutumikia wengine. Kwa sababu hiyo, tamaa ya kazi zetu ambazo hutubidisha zaweza kuwa kitu chema. Lakini kama tutakavyoona siku ya mwisho ya mpango huu kesho, ni pale tuu ambapo bidii yetu inaambatana na kumtumaini Mungu ndipo tutapata pumziko la kweli.
Kuhusu Mpango huu
Biblia inatuagiza kufanya kazi kwa bidii, lakini pia inatuambia ni Mungu-- siyo sisi --anayetoa matunda ya kazi yetu. Kama mpango huu wa siku nne utakavyoonesha, taaluma ya kikristo lazima ikubali mvutano kati ya “kuamini” na “kujibidisha” ili kupata mapumziko halisi ya Sabato.
More