Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano
Pilato akawaambia ... mimi sioni hatia kwake. Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu(m.6-7). Sheria hiyo inasomeka katika Law 24:16,Yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa. Ajabu yake ni kwamba katika upofu wao Wayahudi wenyewe waliangukia dhambi hiyo ya kumkufuru Mungu! Maana wakadai:Sisi hatuna mfalme ila Kaisari(m.15). Na Wayahudi hawaruhusiwi kamwe kumkiri mfalme mwingine isipokuwa Mungu mwenyewe! Mungu ndiye mfalme wetu pia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/