Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 29 YA 31

Hapa kunatolewa mwongozo sahihi wa maisha yaongozayo na kuokoa wengine. Uasherati na ulevi ni miongoni mwa vitu viondoavyo uwezo wa mtu. Matokeo yake ni pamoja na mtu kushindwa kuamua kutenda haki. Badala yake, vitu hivi vinaleta madhara mengine kama kuambukizwa na UKIMWI. Tusikie Neno la Mungu juu ya vitu hivi:Asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno(Kum 17:17).Msiwaoze wana wao [wasio wa watu wa Mungu] binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye(Neh 13:25-26).Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi(Mhu 10:17). Ili kuepuka kudanganywa na kupotezwa na mambo haya, tegemea Neno la Mungu ambalo ni ngao yako. Fanya linavyokuagiza, Tetea na linda haki za wanyonge wote.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/