Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 2 YA 31

Mtume Petro ni mwanafunzi aliyejulikana zaidi kati ya watu walioishi wakati ule. Katika m.17 mmoja anamtambua,akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu?(m.17). Na baadaye wenginewakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo?(m.25). Na mwingine akasema,je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?(26). Lakini Petro akamkana Bwana wake (m.27), ingawa huko nyuma alijidai kuwa na ujasiri na ushujaa mkubwa:Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako. Yesu akamjibu, Je! wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu(Yn 13:37-38). Badala ya kujiamini na kujidai, tunyenyekee na kumtegemea Bwana Yesu tu. Zingatia maneno haya ya Petro:Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu(1 Pet 5:5-10)!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/