Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa YakoMfano
Upanga Wa Roho
Na Mungu mwenye subira saburi na faraja awajalie kunia mamoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Warumi 15:5
“Shetani hutumia muda wake mwingi kujaribu kuwagawanya wanandoa katika ndoa zao. Anafanya hivyo kwa sababu anajua kwamba nguvu za Mungu na utukufu wake waweza kufikiwa na kutukuzwa kupitia umoja.” Tony Evans
Bwana, Yesu alisema maneno haya, “Ufalme wowote ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; na mji wowote au nyumba iliyofitinika juu ya nafsi yake haitasimama,” (Mathayo 12:25). Ninachukua upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu na kukemea jaribio lolote la kuleta au kuendeleza mafarakano katika ndoa yangu. Nyumba iliyogawanyika yenyewe haitasimama, kwa hiyo ninakataa kukubali na kubaki katika hali ya kutofautiana kiakili na mwenzi wangu. Baba Mungu, elekeza mioyo yetu, akili na roho zetu ziwe pamoja mahali ambapo kulikuwepo mafarakano. Neno lako linasema tunapaswa “kufuatia mambo yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi,” (Warumi 14:19). Umeweka wazi. Sisi kama wanandoa tunapaswa kutafuta, kusema na kufanya mambo ambayo ni ya kujengana mmoja na mwingine, ndani yako.
Tupe ufahamu na hekimaya jinsi ya kufanya hivyo. Siwezi kujua siku zote ni nini kitakachomjenga mwenzi wangu ndani yako. Ninaweza kufikiria ni jambo moja na iwe ni jambo tofauti ambalo litakuwa na athari kwake. Kwa hivyo tafadhali Bwana, saidia akili yangu kuelewa, kusema na kufanya mambo ambayo yatamjenga mwenzi wangu ndani yako. Iwe ni maandiko kwa ujumbe mfupi ninayotuma, maneno ninayozungumza au chochote ninachofanya kinachomhusisha mwenzi wangu, acha kiwe ni kitu kinacho chochewa na wewe ili kutujenga na kutuunganisha kama wanandoa chini yako. Katika jina la Kristo, amina.
Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.
Kuhusu Mpango huu
Moja ya matamanio makubwa ya wanandoa ni umoja. Kwa kushangaza, hii imeonekana kuwa ya kuteleza sana. Mara nyingi, tofauti za maoni zinapoingia, matokeo yake ni migogoro, kukata tamaa na kuumia. Katika hali kama hizi, wenzi wa ndoa wanapaswa kusali jinsi gani? Katika kampeni yetu ya siku sita, Sala kwa ajili ya Umoja katika Ndoa Yako, wanandoa wataweza kudai umoja katika ndoa yao, wakifanya hivyo kwa kuomba kulingana na ukweli wa Maandiko. Kila sala inafanana na sehemu moja ya silaha kamili ya Mungu, iliyokusudiwa kuwatayarisha waume na wake kwa ajili ya umoja.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/