Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

SIKU 4 YA 6

Ngao Ya Imani

Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Warumi 12: 4 – 5

"Umoja haimaanishi ulinganifu au usawa. Umoja unamaanisha umoja wa kusudi. Kama vile Uungu unavyofanyizwa na Nafsi tatu tofauti—Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu — kila mmoja wa kipekee katika utu, na wakati huo huo mmoja katika kiini, umoja huonyesha umoja ambao haukanishi hali ya pekee ya mtu.” Tony Evans

Mungu mpendwa, mimi na mwenzi wangu tuna mambo kadhaa tunayofanana lakini pia tuna tofauti kadhaa. Haya huja katika maeneo mbalimbali—Unayajua yote wote. Wakati mwingine ni sawa kwetu kuyashughulikia, lakini nyakati nyingine zingine inakatisha tamaa. Ninapo katishwa tamaa, napoteza imani kwamba hata inawezekana kuwa na umoja wakati ambapo sisi ni tofauti sana. Lakini hukusema kwamba twapaswa kufanana ili tuweze kuunganishwa. Badala yake, umoja wetu unapaswa kuakisi kile ambacho Paulo aliandika katika Warumi kwamba viungo vya mwili wako havina kazi sawa, lakini bado ni mwili mmoja na viungo vya kila mmoja.

Ni rahisi kuelewa umoja na kuwa na imani kwamba tunaweza kuupata ninapoelewa kwamba hauniitii niwe kama mwenzi wangu, lakini badala yake kuwa na nia-sawa na mwenzi wangu, chini yako.

Pale ambapo mitazamo yetu ya kiroho na mitazamo ya maisha hutofautiana, tafadhali tuunganishe chini ya kweli yako. Tunapolinganisha mawazo yetu, imani na maadili chini yako, kiasili tutakuwa na umoja zaidi mmoja kwa mwingine.

Pia, Baba, tusaidie kufurahia na kuruhusu tofauti za kila mmoja wetu kulingana na utu wa kipekee ulizochagua kutupa sisi. Tupe ufahamu tunaohitaji ili kuelewa kwamba umoja haimaanishi kwamba tunapaswa kupenda muziki sawa, matukio au vipindi vya televisheni sawa, lakini badala yake, umoja unamaanisha akili zetu, mawazo, madhumuni ya pamoja na maadili yanahitaji kuunganishwa chini ya Neno lako. Tunapoishi kwa imani tukitumaini Neno lako, tutaunganishwa. Katika jina la Kristo, amina.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

Moja ya matamanio makubwa ya wanandoa ni umoja. Kwa kushangaza, hii imeonekana kuwa ya kuteleza sana. Mara nyingi, tofauti za maoni zinapoingia, matokeo yake ni migogoro, kukata tamaa na kuumia. Katika hali kama hizi, wenzi wa ndoa wanapaswa kusali jinsi gani? Katika kampeni yetu ya siku sita, Sala kwa ajili ya Umoja katika Ndoa Yako, wanandoa wataweza kudai umoja katika ndoa yao, wakifanya hivyo kwa kuomba kulingana na ukweli wa Maandiko. Kila sala inafanana na sehemu moja ya silaha kamili ya Mungu, iliyokusudiwa kuwatayarisha waume na wake kwa ajili ya umoja.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/