Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

SIKU 5 YA 6

Chapeo Ya Wokovu

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani, Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. 1 Wakorintho 6: 19 – 20

"Umoja hutokea tunapounganisha tofauti zetu za kipekee pamoja tunapoelekea kwenye lengo moja. Ni hali ya kuhisi kwamba kitu hicho ambacho kimetukusanyisha na twakielekea ni kubwa kuliko mapendeleo yetu binafsi.” Tony Evans

Bwana, kupitia kifo na ufufuo wa Kristo, ulinipa wokovu wa milele. Yesu aliyatoa maisha yake ili wokovu wangu wa milele upate kulindwa. Ulininunua kwa gharama kupitia dhabihu ya Mwana wako. Kwa sababu ya ukweli huu, nipo ili kukutukuza kwa maisha yangu. Vivyo hivyo na mwenzi wangu. Sisi hatujimiliki wenyewe. Kusudi letu ni kukuletea utukufu kupitia chaguzi zetu, maneno na hali ya mioyo yetu.

Tusaidie kuachilia mapenzi na haki zetu za kuwa na njia yetu wenyewe ili tukuheshimu wewe kwa umoja pamoja. Tupe picha kubwa ya ufalme wako na utukumbushe kusudi letu kuu ambalo ni kukutukuza wewe. Utengano ni uasi kwa sababu utengano huweka matamanio na mapenzi yangu juu ya yako. Mgawanyiko unasema ninaweka madai ya maisha yangu, mwili wangu na chaguzi zangu bila kujali dhabihu ya Kristo na zawadi yako ya wokovu kupitia msamaha wa dhambi.

Umoja huakisi mioyo ya kujisalimisha chini yako, Bwana, jambo ambalo Neno lako linasema tufanye kwa msingi wa ukombozi wa Kristo kwetu. Utupe ukumbusho huu wakati mambo yanapotengana katika ndoa yetu, na utuwezeshe kushinda changamoto zinazotukabili ili tuweze kuunganisha mioyo yetu katika upatanisho chini yako. Katika jina la Kristo, amina.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

Moja ya matamanio makubwa ya wanandoa ni umoja. Kwa kushangaza, hii imeonekana kuwa ya kuteleza sana. Mara nyingi, tofauti za maoni zinapoingia, matokeo yake ni migogoro, kukata tamaa na kuumia. Katika hali kama hizi, wenzi wa ndoa wanapaswa kusali jinsi gani? Katika kampeni yetu ya siku sita, Sala kwa ajili ya Umoja katika Ndoa Yako, wanandoa wataweza kudai umoja katika ndoa yao, wakifanya hivyo kwa kuomba kulingana na ukweli wa Maandiko. Kila sala inafanana na sehemu moja ya silaha kamili ya Mungu, iliyokusudiwa kuwatayarisha waume na wake kwa ajili ya umoja.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/