Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Yusufu alifika mbele ya Farao pamoja na baba yake na baadhi ya ndugu zake. Alikuwa ameshawafundisha namna ya kumjibu Farao akisema, Itakuwa Farao atakapowaita, na kuwauliza, Kazi yenu ni nini? Semeni, Watumwa wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu. Yusufu aliwaambia pia sababu ya kusema hivyo: Mpate kukaa katika nchi ya Gosheni (46:33-34). Yusufu alijitahidi kumpendeza Farao ili awatendee mema. Farao alimwuliza Israeli juu ya umri wake. Israeli akajibu, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni 130; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu (m.9). Israeli alikuwa msafiri. Hakuona raha idumuyo. Alitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni! Ni kama ilivyoandikwa katika Ebr 11:9-10: Alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/