Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Raheli alikuwa amefariki mapema, kwa hiyo Yakobo alipata wana wawili tu kwake, Yusufu na Benyamini (m.7). Ila sasa wakawa wanne, maana Yakobo aliwafanya wana wa Yusufu kuwa wana wake yeye mwenyewe. Ndivyo anavyomwambia Yusufu katika m.5, Sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni. Hivyo taifa la Israeli likawa na makabila 13, Yusufu akigawanyika katika makabila mawili, yaani, Efraimu na Manase. Baraka ya Mungu kwao ilikuwa hasa kwamba wataongezeka kuwa wengi sana (m.16, Wawe wingi wa watu kati ya nchi). Na kweli, kwa pamoja wao wakawa wengi kuliko kabila lingine. Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba; … hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao (Hes 26:34 na 37)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/