Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 23 YA 30

Huko nyuma Yusufu alikuwa ameonyesha moyo wa kuwasamehe ndugu zake (45:4-8). Lakini baada ya kifo cha Yakobo ndugu zake wakawa na wasiwasi kwamba huenda aliwasamehe tu kwa sababu ya baba yao, wakasemezana, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye namna hiyo (m.15-17). Tendo hili laonyesha kuwa kusamehe kwake kulikuwa kwa moyo. Inaonekana pia katika yale anayosema nao. Maneno yanafanana na yale ya huko nyuma. Akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema (m.18-21). Kibinadamu isingaliwezekana! Lakini alikuwa na Roho wa Mungu ndani yake! Zingatia ilivyoandikwa katika Rum 12:19-21: Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/