Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Yusufu alijitahidi kuwaweka wana wake ili mzaliwa wa kwanza abarikiwe kwa mkono wa kuume wa Israeli (m.13). Alipoona baba yake anafanya kama isivyotakiwa, akataka kumzuia akisema, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake (m.14 na 17-18). Lakini Israeli akakataa, akasema, Najua, mwanangu, najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa (m.19). Na kweli, baadaye kabila lake Efraimu likawa ndilo lenye nguvu kati ya makabila mengine ya kaskazini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/